Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
JK atakuwa kwenye wakati mgumu sana safari hii, kwani ukiangalia kwa undani(kina) hii ni dosari kubwa sana kisiasa kwake na CCM hata hizo safari zake za mara kwa mara za nje zitapunguwa maana atakosa lakujibu pindi atakapoulizwa juu ya hili la CHADEMA kususia shughuli zake zote ikiwamo kutomtambua kama Rais wa JMT
 
Kashalikoroga cha ajabu anaogopa kulinywa

Hapakaliki mjomba, maana moto alouswasha unamuunguza atiii!!!!
 
hawa si ndio walidhamini tangazo la udini kupitia ikulu kama ilivyolipotiwa na raia mwema?

Alafu huu udini wanaohubiri mbona hawatoi evidences watu wanaishia kusema udini udini bila kusubstantiate where
si walituma msg kuwa slaa ni mdini hatakiwi sasa wajisafishe wenyewe pumbaa&&&&fu senu!
 
Inasikitisha sana kuona wakati kila Mtanzania yuko bize na mambo yake lkn JK anabaki kupiga kelele kuwa kuna hisia za udini zimejengeka kwenye jamii. Akumbuke kuwa kila analoongea hata kama halikuwa kwenye mawazo ama akili za watu wakati mwingine linawafanya watu waanze kutafakari kwa undani. Inakuwaje tangu alipokuwa anafanya kampeni suala la udini amekuwa akiliongea yeye na wenzake kwenye club yao? Mbona anataka kuwafanya Watanzania waanze kuhisi kuwa kuna jambo limefichwa nyuma ya pazia! Kuna mambo mengi yanahusu mustakabali wa Taifa hili lkn JK kwake udini ndiyo ameona jambo la kushikia bango, inatakiwa kuwa makini ktk hili vinginevyo kuna wingu zito liko mbele yetu.
 
Watatu waliopewa ubunge!!!!!!!??????
 
Leo Tendwa amenikera sana na kauli zake ati CHADEMA kwa ku-walk out wamevunja katiba....hata Obama ali walk-out Ahmedinajad alipohutubia UN
 
Ujumbe nilioupata ni kuwa JK jana alikiri kuwa Dr. Slaa alimshinda kwenye uchaguzi kwa sababu wakristu ni wengi na walimpigia mkristu mwenzao...ila na yeye ilibidi atumie nguvu za ziada za dola kuhakikisha anayachakachua matokeo ya kupigakura kwa misingi ya udini..................Haya maono yangu yanasababishwa na yafuatayo......................kama JK alipata kweli asilimia 61 mwaka huu je hao waliompigia kura siyo wakristu? Hao waliompigia kura asilimia 81 mwaka 2005 hao wakristu hawakuwemo? Ukweli ni kuwa mwaka 2010 hakuzipata hata hizo asilimia 61 na ndiyo maana analaumu udini badala ya kulaumu uwezo wake wa kiuongozi ni duni mno......yaani hata unatia kichefuchefu, vile.......

Mbona mwaka 2005 hakulalamikia udini na chaguzi hii huu udini kauanza wakati wa uchaguzi huu tu kabla ya hapo mbona alikuwa haoni? Hii ni baada ya Dr. Slaa kumwonjesha joto la jiwe.......

Sisi kumchagua Jk mwaka 2005 tulifikiri ana uwezo.........................siyo kwa sababu ya dini yake na tulipomkataa mwaka 2010 si kwa sababu ya dini yake ila tulimkataa JK kwa kuubeba ufisadi tu...............................na hivyo kutuongezea umasikini.....................Will the real JK rise up and be counted among the great inspirational leaders of this nation?

My fear is he will never rise up to the occasion..........................
 
ASANTE SANA mwanakijiji ila inasemekana siku zako zinahesabika , jiangalia brother

mwanakijiji doesn't exist, it is a figment of imagination na hao wanaomtafuta they will end up chasing wind
 

Suleyman Kova????
 
Kwakweli nimechefuka sana kusikia eti Rais wa nchi anasema kuna nyufa za udini. Huu udini umetoka wapi? Mimi ninavyofahamu ni kwamba mambo ya udini huwa yanaanzia mitaani kwenye jamii tunamoishi. Sasa kama tunaishi kwa amani kwenye neighborhood tatizo ni nini? Au huo udini uko Ikulu? Nani aliyemshauri kutoa maneno kama hayo? Walianza na ukabila naona sasa wameshindwa coz CHADEMA inakubalika TUKUYU HADI BIHARAMULO. Je Udini ni upi kama sio kushughulikia uanzishwaji wa mahakama ya KADHI kama alivyosema makamu wa Rais?
 

HUPO SAWA KABISA, ni lazima CHADEMA watuambie wameibiwaje ibiwaje kura zao. kura sio saa au simu yako maana simu au saa kamauliiweka ndani mwaka ukafunga mlango uliporudi ukukuta pale ulipo weka hata ulipotafuta ukuvipata vifaa hivyo waweza kutamka bila shaka kuwa umeibiwa vifaa vyako. Lakini sio suala la KURA inahitaji ushahidi yakinifu kutushawishi kuwa umeibiwa, ushahidi ambao wengi tunasimamia ni ushahidi wa kimazingira. Maadam CHADEMA mmesema mnaushahidi halisi wa kuibiwa kura uwekwe wazi ili kila mtu auone na tumtie aibu Jaji Makame, Rajabu Kiravu na JK pamoja na CCM na wanachama wake. Hiyo itasaidia sana katika mapambano ya kumkataa rais aliyepo madarakani lakini kinyume chake ni hushaidi wa kimazingira uliopo unaonyesha kama suala hili ni uzushi maana kila mtu ataelezea kilichojili jimboni kwake, na alichosimuliwa na jamaa zake kuhusu kilichojili majimboni mwao.

Mfano Mimi nakubaliana na dhana ya kuibiwa kura maana natoka ktk jimbo la Segerea na kilichotokea wengi wetu mnakijua na MPENDANZOE kaenda mahakamani lakini wa jimbo la HAI wanaushaid gani maana si kulalama tu kuwa kura za MBOWE zilizidi za SLAA sio ushahidi yakinifu. jamani sio tukikuta watu wanalia tunaanza kulia na sisi baadae tukiulizwa tunalia nini tunabaki tumeduwaaaaa ......... CHADEMA tupeni majibu mapema ili tuwajuze watanzania wenzetu kwa ushahidi makini na halisi pia Tuwe na hoja nzito hata kwa JUMUIA YA KIMATAIFA maana wameshuhudia kutokwa kwa CHADEMA Bungeni wakitaka kujua shida ni nini tuwe na ushahidi makini na halisi wa kutetea kuibiwa kwetu
 
CHADEMA sio kwamba wanapingana na JK na matokeo yake bali pia wanapingana na KATIBA ya JMT sasa. Baadhi yetu tuliwaambia mapema kuwa kwa kuwa KATIBA ni ileile, NEC ni ileile, WATANZANIA na CCM yao ni walewale, Vyombo vya DOLA ni vilevile, kusingekuwa na namna ya kumshinda JK labda wangempunguzia kura tu.
Jana walipooondoka kwenye viti vyao mle Bungeni tu, CUF, NCCR-MAGEUZI, TLP wakazichukua zile nafasi haraka kama vile walizitarajia. Tuna safari ndefu ya kuleta mabadiliko TANZANIA.
 
1. Kikwete ni rais wa kwanza Tanzania kuzomewa na wananchi katika ziara ndani ya nchi.

2. Kikwete ni rais wa kwanza Tanzania kukumbwa na malumbano na wafanyakazi mara kwa mara

3. Kikwete ni rais wa kwanza Tanzania kuanguka jukwaani

3. Kikwete ni rais wa kwanza Tanzania kususiwa na wabunge bungeni

God knows what else this guy has in store for us
 
Tatizo la wengi hapa ni copy and paste, na hii ndiyo shida ya Watanzania wengi. Mama Akilimali kasema, basi watu wanaendeleza hayo hayo. Leteni uchambuzi wenu. Uchaguzi umemalizika, na tuchape kazi sasa.:bowl:
 
nkojo apo ndepolikhe! Funga magazeti yoote yaliyoeneza udini!
 

4: Kikwete rais wa kwanza asiyejua ni kwa nini amekuwa rais na anatakiwa kufanya nini
 
Ni rahisi kusema; mbona mbona walishindwa kupora kwa nguvu majimbo ya mijini-MSM,MZ,MBY,IRA,MHI,ARU UBUNGO, KAWE????????????????? Ngoje Pipooooooooooooooooos Pawaaaaaaaaaaaaaaaaaas bado inkusanya nguvu itakayowabomoa mbele za macho ya jamii ya kimataifa ndipo mtajua uchungu wa kupora haki!!!!!!!!!!!!!! Ndipo mtaona machungu wa yanayompata fisadi mugabe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Yeye ndiye mdini mkubwa!! Message za simu alizokuwa akizituma za kumponda Slaaa kwa udini si zake??
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…