Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
tatizo la chadema wana wivu wa kike!

Kwa mtu yeyote mwenye uchungu na nchi yake, anayetambua mchakato wa uchaguzi ulivyokuwa hadi mshindi kutangazwa na aneyeifaham ya Tanzania lazima ataelewa Chadema kwa kile wlicho kifanya. Ila kwa mtu asiyejitambua, anaeishi kwa sababu asubuhi ya siku nyingine imefika, fisadi au mwenye masilahi binafsi na CMM au yule asiye na uelewa na mstakabali wa taifa letu, atasema maneno mengi mabaya juu ya chadema na hata kusema kama wewe kuwa Chadema wana wivu.

JK anatambua wazi kuwa hakupata ushindi uliotangazwa na NEC, hivyo anajaribu kuondoa fikira za watanzania kutoka katika madudu ya Uchaguzi na kuwapeleka kwenye udini na ukabila ambao anauhubiri kwa nguvu hivi sasa. Jamani wa TZ kuna ukabila ambao JK anauhubiri hapa nchini kwetu?

Chadema wako sahihi na kila mwenye kuelewa analitambua hilo. Mwenye masikio na asikie
 
Wamejaa washabiki ya chadema JF, uwezi kupata mjadala wenye matiki hapa....
 
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.

Mmh!wewe nawe!
 
- Wakuu kuuliza si ujinga ninauliza hivi: Chadema wana tatizo na NEC kwa sababu kikatiba ndio wenye mamlaka ya kuamua nani awe Rais kutokana na kura za wananchi walizonazo mikononi,

- Au wana tatizo na Rais kwa sababu amewaibia kura ambazo zinaonyesha kwamba Dr. Slaa ndiye aliyeshinda U-Rais?


William.
Hawaelewi tatizo hasa nini? Nadhani hawajatambua hasa wanataka nini?
 
Kwenye uchaguzi huu hata CHADEMA wamepata wabunge wengi kumbe nao wamechaguliwa na NEC?

Wewe mwenzetu vipi? Mbona hamjawasusia kama wamechakachua au muwapeleke mahakamani? Mi nadhani umemrithi Malaria sugu ambaye haponi malaria.
 
Kuna watu humu siwaelewi, sijui wao anatakaje ! NEC imemchagua raisi, na dola lina msikiliza, kumpinga mlitaka watu wafanyeje ! aende ikulu na mapanga ? Dr. kaelezea kuwa mapambano yatakuwa kwa amani na ustaarabu, chadema hawana mabavu ya kijeshi au ya kidola kuweza kuafanya wanyangányi wa kura za watu wawarudishie uma haki zao isipokuwa kwa kutumia njia alizo zielezea. Sasa kama nyie mnaushauri mwingine mzuri zaidi basi na muutoe humu tuujadili.
 
Naamini hii ni transcription rasmi ya taarifa ya Dr Wilbroad Slaa……

Ndugu zangu Watanzania, pamoja na ndugu zangu wote waliokuwa wanafuatilia matukio ya bungeni leo. Aaah... ni kweli nimepata watu wengi wakiulizia, aah.. ni kwanini wabunge wa CHADEMA walitoka ndani ya ukumbi wa bunge, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano alipoanza kutoa hotuba yake.

Hivi wabunge wa Chadema si wana uongozi wao na msemaji wa makubaliano ya caucas yao ni ama Mwenyekiti wa chama ama Mnadhimu wa wabunge (Party Whip). Hatua ya Dr Slaa kuliongelea hili sio uthibitisho kuwa hatua hii ni shinikizo lenye kujali maslahi yake (EGO) na sio maoni ya wabunge wa CHADEMA? Katibu wa chama anawezaje kuwa msemaji wa msimamo uliotolewa na kikao cha wabunge ambacho yeye sio msemaji wake?

Eeenh... moja ni kwamba CHADEMA ni chama chenye msingi, kinachofuatilia, eenh na kuhakikisha kwamba daima kiko consinstent yaani kinatekeleza kile ambacho kinasimamia, aah kwa kuwa tulikwisha kukataa kutambua matokeo ya uchaguzi, na vilevile baada ya kukataa kutambua matokeo tulikataa vilevile kumtambua rais aliyepatikana kwa mchaka.. eenh kutokana na mchakato huo ambao hatuutambui, basi ni dhahiri kabisa aah matendo yetu yaendane na kile tunachoamini.

Nini msingi wa CHADEMA…ni miaka mitano sasa najaribu kupata jibu ya swali hili nashindwa?

Wabunge wetu wapo kwenye forum ambayo inasimamia kile ambacho CHADEMA inakiamini. Bunge ni mahali ambapo wabunge wana nafasi ya kubeba bendera ya CHADEMA, na mahali pa kwanza pa kuonyesha kwamba hatumtambui rais ni dhahiri basi ni kwamba ni ndani ya bunge.

I hope kuna kitu mnakiaamini ziadi ya kuwa ninyi ndio wateule wa kutawala nchi ya Tanzania na sio wengineo kama ambavyo baadhi ya wagombea wenu walivyokuwa wakijinadi kwa kuchakachua tafsiri za maandiko matakatifu……..

Kitendo cha leo kilianzia asubuhi, kwa wabunge wetu kutohudhuria hafla ya kumuapisha Waziri Mkuu, kwa sababu isingekuwa na maana kwenda kuhudhuria hafla ambayo inasimamiwa na rais ambaye kimsingi hatumtambui, lakini vilevile ni ishara kwa watanzania kwamba bado eenh tunataka maelezo ya kina kutoka serikali kuhusu kauli tulizokwishakuzitoa.

Kama hamumtambui Rais iweje mpige kura ya hapana kwa uteuzi wake na sio kutoshiriki katika hatua hiyo kwani Waziri Mkuu huyo ni mteule wa Rais msiyemtambua?

Hizi ni ishara muhimu katika siasa, kupelekea kuipeleka kwa serikali kwamba kuna malalamiko ya msingi ambayo tunayo kuhusu mchakato wa uchaguzi, na ni dhahiri kwamba kama serikali ni makini, kama serikali ni sikivu basi itasikiliza kauli hiyo ya wenzetu ambao huko bungeni. Lakini kauli hizo hazitaishia pale, kama tulivyokwishakutoa katika press conference yetu, tulisema tutatumia forum ndani ya bunge, na forum nje ya bunge kupiga kelele mpaka serikali itusikilize.

Kwangu hii ni ishara ya kuwa mnadhani kuwa siasa za DRAMA na EMMOTIONS ndizo zilikuwa mtaji wa mafanikio yenu katika uchaguzi huu na sio siasa za engagement kama ambavyo mlikuwa mkizifanya katika miaka kumi iliyopita na hivyo kuwajengea imani njema miongoni mwa baadhi ya watanzania wengi wao wakiwa bado wanajitambulisha kama CCM haohao ambao mnaonysha sura ya kuwa wao ni maadui zenu……I hope u have what it takes to be 100% protest party in a conservative socity like ours ambayo in miaka 50 ya kuwa shaped na fikira na mitazamo ya CCM…..

Lakini pia sidhani, siamini na wala sitegemei kuona serikali MAKINi inakubali kuwa blackmailed kama ambavyo mnafanya….Hiyo itakuwa ni serikali joga na sio serikali makini. Kwangu mimi ingawa serikali hii na kwa miaka iliyopita ilikuwa na mapungufu mengi sana lakini naamini na natambua kuwa ilijitahidi kwa kiasi kikubwa kuwa sikivu hata kama sio kwa kila kitu mlichotaka ama watanzania walikitaka.

Lakini hivi tangia lini matendo ya wabunge 47 ya kumvunjia heshima kiongozi wa wabunge 250+ yakaweza kushinikiza siasa za usikivu ama umakini na sio vice versa? Kama miaka 15 ya siasa kama hizo kati ya CUF na CCM ambao ni wazi historia na mgawanyiko wa kijamii wa zaidi ya miaka 50 uliwafanya kuwa na nguvu sawa kiushawishi zilishindwa hadi upande moja ulipolazimika kuwa na uthubutu wa kumheshimu mwenzie ndipo tunaona yanayotokea Zanzibar. Hivi ninyi ambao ukweli ni kuwa ushawishi wenu umegawanyika katika asilimia 10 ya wafuasi na 15 ya washabiki, na wenzenu ni dhahiri wana ushawashi wa zaidi ya asilimia 60, mnategema kweli kuna uwezekano wa kufanikiwa kulazimisha UMAKINI mnaoujengea mazingira kwa style hii? Ama wenzetu mnategemea mgawanyiko wa kijamii ambao umekukuzwa sana na harakati za uchaguzi utastawi na kuwawezesha kuongeza political base ya kuilazimisha CCM kusalimu amri hivi karibuni?

Ni nini tunachokihitaji ? Tunahitaji, aah, demokrasia ya kweli katika nchi yetu, tunahitaji uchaguzi ambao utaendeshwa kwa misingi ya misingi ya demokrasia ya kweli.

Nadhani the best way ni kuanza na demokrasia ya kweli katika CHADEMA. Angalao kufanya uchaguzi mmoja bila ya uchakachuaji wa aina moja ama nyinge kama uzoefu unavyoonyesha. Nasema hivi kwa kuwa hata kama serikali iliyopo madarakani italeta mabadiliko ya aina gain, kama CHADEMA na vyama vingine hamjaweza kuheshimu na kujenga utamaduni wa demokrasia ya kweli katika platform zenu basi daima hamtaweza kuenga imani ya kuwepo kwa demokrasia ya kweli hadi pale demokrasia hiyo itakaporidhisha maslahi yenu binafsi na kukandamiza maslahi ya wengine ambao mnadhani kuwa demokrasia ya sasa inawapendelea.


Tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Eenh.. tunahitaji sheria mbovu ziweze kurekebishwa, ili chaguzi zisiendelee kuchakachuliwa kama ilivyotokea safari hii. Kwa hiyo haya ni mambo ya msingi ambayo hakuna mtu yeyote atatuambia tusiyadai, kwa sababu tumelalamika mara nyingi juu ya kat.. ya marekebisho ya katiba, serikali imekuwa si sikivu haitaki kusikiliza, tumedai kuhusu tume huru, serikali imekataa kutusikiliza,

Hapa nakubaliana nanyi asilimi mia moja, Katiba mpya ni muhimu sio kuwa ndio utakuwa ukombozi wa mtanzania lakini zitaondoa ama kupunguza athari za siasa za hisia ambazo zinawezeshwa na utata wa uhalali wa utungaji na ubadilishaji wa katiba yetu…….Tume huru pia ni muhimu laki uhuru huo usiwe hadi pale tu "mtakaporidhika" kwa misingi ya maslahi yenu bali uhuru ambao utawaruidhisha watanzania kwa msingi wa maslahi ya watanzania wote wakiwemo wale walio CCM na wale tusio waamini ninyi nyote….

tumedai marekebisho ya sheria mbalimbali ambazo ni kandamizi serikali haitusikilizi,

Hivi katika sheria arobaini ambazo Jaji Nyalali alizitambua kama sheria kandamizi ni ngapi zimeondolewa, kubadilishwa ama zimebaki? Hivi mnaposema sheria kandamizi ni zipi hizo? Zitajeni tuzijue na kuzielewa sio kutuburuza tu kuwa kuna sheria kandamizi……

Itaendelea..........
 
Timu kamili ya udini imekamilika bunchan, Henge, safari_ni_safari, Baba_Enock na wengine wengi humu ndani. Lakini cha ajabu hao ndio senior expert members hapa JF.
JK mnadai ni mdini (inaweza kuwa kweli au sio kweli),lakini nyie kwa michango yenu hapa JF mmeonyesha chuki zenu za udini without shame, sio kwamba mnasingiziwa. It says a lot about JF members.....
 
tatizo la chadema wana wivu wa kike!
Wee mwanamke mwanamume? Unahitaji kutoa hoja tu :angry:. Kilichofanyika ni kupeleka ujumbe na wananchi tumeridhia. Na kwa taarifa hili sasa ni gumzo la kimataifa, mlidhani mnaendesha mabwege, poleni CCM.
 
Katika mambo ambayo JK ameyaongea kwa msisitizo na sauti ya kimadaraka ktk hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge, ni suala la UDINI, kuwa udini unaanza kujitokeza.

Naomba mnijuze wapambanuaji, ni nini kimetokea mpaka JK alikemee kwa sauti kubwa kiasi hicho suala la UDINI? Je ni kwasababu matokeo ya uchaguzi hayakufika 80% kama walivyotarajia? Au kuna sehemu wakati wa kampeni na hata uchaguzi huu, kulitokea UDINI? Nionavyo mimi, tamko lake hilo, laweza kuleta mka'nganyiko kwa wananchi.

Natoa hoja.
I also have pondered his speech and especially the 'udini' issue, i really dont see it maybe this is me, but in any case advocating for it will now make us raise our well worn eyebrows, this activist who immediately preceded after TBC news couldnt have said it any better..
 
CHADEMA sio kwamba wanapingana na JK na matokeo yake bali pia wanapingana na KATIBA ya JMT sasa. Baadhi yetu tuliwaambia mapema kuwa kwa kuwa KATIBA ni ileile, NEC ni ileile, WATANZANIA na CCM yao ni walewale, Vyombo vya DOLA ni vilevile, kusingekuwa na namna ya kumshinda JK labda wangempunguzia kura tu.
Jana walipooondoka kwenye viti vyao mle Bungeni tu, CUF, NCCR-MAGEUZI, TLP wakazichukua zile nafasi haraka kama vile walizitarajia. Tuna safari ndefu ya kuleta mabadiliko TANZANIA.

..safari ndefu ya wapi? ww bado una amini cuf wana mchango wowote huku serikali ya muungano? umechelewa! fikiri tena! think people should know that we hv to stand fr our territory right now! ukisubiri kufanya maamuzi kwa kuwatizama cuf ni km unasubir watu wa pemba waje kukusaidia kwa matatizo uliyonayo! lakin je ww uliwasaidia nn hata wkt ule baadhi yao wanakimbilia mombasa, yaani ule uchaguzi wa 2000? hp jibu unalo km dhamira ya kuondokana na uchaguzi wa kihuni kam wa safari hii ipo!
 
Hiyo kauli ya kichwa cha habari imetoka wapi? Kwenye hotuma Mh JK sijasikia kitu kama hicho
 
Dr., Since umeanza kwa kuongelea consinstency, swali langu mimi ni, kama hamumtambui Kikwete mlipopiga kura pendekezo lake bungeni kwa kiti cha Waziri Mkuu, mlikuwa mnapigia kura pendekezo la nani? Je pale mlimtambua halafu mkashauriana na sasa hamumtambui? Kuna consistency gani hapo ?



Utasemaje unaonyesha kutomtambua rais kwa kutohudhuria hafla ya kuapishwa Waziri Mkuu wakati umehudhuria, kushuhudia na kushiriki upigaji kura zilizompitisha huyo waziri mkuu aliyependekezwa na rais ? Kipi muhimu, kura za kumpitisha au tafrija ya kumpongeza baada ya kupitishwa ? Hivi kweli mnataka tuwachukulie seriously kwa mwendo huu ?



Muda wa ishara umekwisha, tunataka matendo yenye lengo la kuleta mabadiliko ya kisheria.



OK, kwanza unasema serikali haiwasikilizi, halafu unaendelea kusema unategemea serikali itawasikiliza, au hata inaweza kuwaahidi marekebisho. Wanasema kufanya kitu vile vile na kutegemea matokeo tofauti ni kichaa, sasa CHADEMA mnafanya nini tofauti na nyuma ? Au "mnapiga makelele" tu kama unavyosema mwenyewe mkitumaini CCM wataona haya na kuwapa mabadiliko katika kisahani cha dhahabu? Kama hawana haya na hawawapi mabadiliko je, mtafanya nini ?



Again, huwezi kushiriki kumpitisha Waziri Mkuu, halafu ukasusia hafla, halafu uniambie uko serious. This is a big joke.



Mimi ningekusifu na kukupongeza zaidi kama ungesusia kila kitu cha rais huyu, pamoja na kupigia kura uhakiki wa chaguo lake la waziri mkuu.



Njia unayotumia wewe haizai matunda, actually ni the worst of both worlds. Wataka mabadiliko wa kweli kama mimi tunakuona haufanyi vya kutosha, wapenda ushirikiano wa vyama vya kisiasa watakuona unawagawa Watanzania kwa misingi ya vyama. Utawapata wafuasi wako hao hao wanaoamini CHADEMA kama dini.

Kama kweli unataka kutomtambua rais huyu itisha migomo na maandamano nchi nzima.

La, mkubali uende kutaka mabadiliko bungeni. Zaidi ya hapo unazua maswali mengi kuliko majibu.

Rafiki, KIRANGA;

If you take this on the scale of LEGAL FRAMEWORK, you may undermine CHADEMA that they are wrong and what they are doing is wrong, totally wrong as you seem to convey your message. However, if you happened to take a bit of CIVICS OR siasa subject at A-level, you would realize that not all political issues can be solved using the current laws, they may have to be solved polically. Once they are solved polically, the solution becomes the basis for a new LAW. This means that POLITICS is the mother of LAWS and when you mess up politics, most or all of the laws become inner and sticky!

In Kenya for example, the law was not applicable after the last General Elections. They had to use political approaches. After then, new laws were born, HENCE THE NEW CONSTITUTION.

I think CHADEMA's appproach is very scientific, wise, caring and of humanity level. Blaming CHADEMA could have been justified if they tried to express their view violently. Remember, these are Tanzanians as ourselves, brothers and sisters....
 
Mkandara,
Thanks. Nadhani message ya Wabunge na ya kwangu iko very clear isipokuwa kwa mtu anayetaka tu kui spin au kuibadilisha kwa sababu anayoitaka mwenyewe. Naomb kurejea mambo ya msingi kwa wale ambao kwa bahati mbaya yamewapita na wana nia ya kuelewa ili spinning hii isiwabughudhi.
i) Mara baada ya uchaguzi, tarehe 3 November, 2010 Dr. Slaa alifanya Press Conference Makao Makuu ya Chadema kama Mgombea Urais ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi na Matokeo yaliyokuwa yakitolewa kupita Vituo vya TV na Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika Press Conference hiyo Dr. Slaa alitaja dosari nzito katika mchakato wa uchaguzi na hasa katika hatua ya kujumlisha na kutangaza Taifa ambapo matokeo yaliyokuwa yakitangazwa na NEC yalitofautiana kwa kiwango kikubwa sana na yale yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi (W) pale ambapo zoezi hilo lilifanyika. Nikatoa Mfano wa Geita. Pili, nilieleza kuwa Katika majimbo takriban 25 zoezi la majumlisho halikufanyika kama inavyotakiwa na sheria na hivyo matokeo kutangazwa na wasimamizi kwa utaratibu kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi. Tatu, nilieleza kuwa katika maeneo mengine kama Kinondoni masanduku yapatayo 25 ambayo tunayo namba zake tunazo yalipatikana katika ghala la Shule ya Sekondari ya Biafra Jijini Dar-Es-Salaam ambayo hayajahesabiwa na matokeo yamekwisha kutolewa.Nne, Siku ya tarehe 28 October, Tume ya Taifa ya uchaguzi ilialika Wataalam wa IT wa vyama, na kuwa mbele ya Wataalam hao mfumo wa computer uliokuwa unatumika uli "collapse" na Tume kuwajulisha Wataalam kuwa wataita LapTop zote kutoka nchi nzima zirejeshwe Dar kwa matengenezo ya program husika. Ni kuwa wataitwa tena kujulishwa kama zimetengenezwa. Hawakuitwa tena. Hivyo mfumo wa Computer uliotumika kukusanya matokeo na upeleka Taarifa NEC unatia mashaka makubwa.Hata hivyo,baadaye tulipokea Barua kutoka NEC ya tarehe 28/10 ambayo ililetwa kwa Dispatch Makao Makuu Chadema tarehe 5 November, ikisema " Watalaam walikuwa na kukagua mfumo wa IT unaotumika na Tume na waliridhika" . Ni dhahiri barua hii inatia mashaka kwanini barua ya tarehe 8/10 iletwe kwa dispatch na ifike siku takriban 8 baadaye? Hali hii inatia mashaka kuwa barua hii imekuwa backdated kwa Tume kuficha ukweli wa Scandal kubwa iliyotokea katika mfumo ambao uligharimiwa kwa fedha nyingi na UNDP. Iwapo Tume inaweza kudanganya katika swala kama hili tutatukuwa na imani gani na Tume tena. Kutokana na dosari hizo kubwa (pamoja na mambo hayo yaliyojitokeza baadaye) Dr. Slaa, kama Mgombea aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye mambo yafuatayo:
i) Kusimamisha Zoezi la Kutangaza matokeo hadi uchunguzi kamili utakapokuwa umefanyika ili kuondoa hisia na tofauti zilizoanza kujitokeza. Ikumbukwe kuwa Tofauti hizi kimsingi ziligundulika na Wananchi wenyewe kutokana na Tarakimu alizosoma Jaji Makame kutofautiana na zile zilizotangazwa na Wasimamizi katika maeneo yao. Matokeo yake wananchi waliingia mitaani kupinga hali hiyo. Hayo yalitokea Geita, Shinyanga, Mbozi Mashariki na kadhaa. Matokeo yake wananchi hao waliokuwa wanadai haki zao walipigwa mabomu na polisi. Njia ya Busara ilikuwa kuitaka Tume kusitisha zoezi hili ili lisilete athari zaidi, japo hawakufanya hivyo. Chadema tulifanya jitihada za ziada kuwasihi wananchi wetu wasiingie mitaani kuepusha shari. ii) Kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuta uchaguzi na kutangaza upya marudio ya uchaguzi kwa kuwa Tofauti zilizoko ni kubwa sana, na nikatoa mfano wa Tarakimu za Geita CCM 17,792 CDM 3,789 ( Iliyotangazwa na RO Geita CCM 30,960 CDM 22031) Ni wazi kilichotokea hapa ni kuchakachua kwa lengo la kupunguza kabisa kura za Dr. Slaa, japo za JK nazo zimepunguzwa). Jimbo la Hai CCM 35,910 CDM 18,513 (Iliyotangazwa Hai na RO CCM 20,120 CDM 26,724 = Uchakachuaji uliofanyika hapa ni wa kumwongezea JK kwa zaidi ya kura 15,000 na kupunguza za Dr. Slaa kwa zaidi ya 8,000). Nilitoa pia mfano wa Ubungo ambapo kwa mujibu wa CCM 68,727 CDM 65,450(iliyotangazwa na RO CCM 70,472 CDM 72,252 hapa nako uchakachuaji ulioafanyika ni wa kupunguza kura za Dr. Slaa kwa Takriban 8,000 na kupunguza za CCM kwa kama 2000 hivi) Katika Jimbo la Bunda CCM 20,836 CDM 571 ( Iliyotangazwa na RO CCM 20,836 CDM 18,445 = Tarakimu za Bunda zimerekebishwa katika Taariffa ya mwisho ya NEC. Taarifa hii inaonyesha kuwa Dr. Slaa alipewa kura za Lipumba). Jimbo la Karatu ni kichekesho zaidi kwani kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya NEC iliyonukuliwa na Mwananchi CCM 24,364 CDM 41 ( iliyotolewa na RO CCM 24,364 CDM 43,137. Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu. Tume ilikiri kuwa imekosea Taarifa ya Geita japo hadi leo haijarekebisha Taarifa hiyo.Hadi leo hii tarehe 19/11 Tume haijatangaza matokeo ya Geita, Tumbe, Tunduru Kaskazini, na Vunjo kwenye Website yake. ( Tume ilikiri siku ya kujumlisha matokeo Taifa kuwa Vunjo kulikuwa na Taarifa mbili na ikaamua kutumia ile ambayo haikusainiwa na mawakala na kutumia ambayo haina saini ya mawakala. Ni akili ya kawaida tu kujua kuwa kuna jambo hapo.
Hivyo basi kutokana na Dosari hiyo kubwa mgombea yeyote anayekubali kupokea matokeo atakuwa mwendawazimu. Ndiyo maana nikakataa kutambua matokeo na kumtambua Rais aliyepatikana kwa matokeo hayo.

2:Tarehe 15 November, katika Press Conference iliyofanyika Dodoma, Dr. Slaa, alikabidhi rasmi majukumu kwa Chama kwa kuwa kazi ya Mgombea Urais imefikia mwisho wake Baada ya Rais kutangazwa kwa mujibu wa Katiba (Mbovu) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa chombo ambacho kilikasimiwa madaraka na Kamati Kuu ya Chama ( Sekretariat) mbele ya Wabunge wa Chama. Chama kilipokea majukumu na kuelekeza utekelezaji na ufuatiliaji maazimio hayo ya kukataa matokeo na kumkataa Rais kufanyika kuanzia siku hiyo na Vyombo mbalimbali na ngazi mbalimbali za Chama, na Wabunge wa Chama. Hivyo kilichotokea Bungeni ni utekelezaji wa maamuzi ya Chama hadi pale ngazi za juu za Chama zitakapobariki au kubadilisha msimamo huo. Ni dhahiri basi, i) Wabunge wetu wala Dr. Slaa, hawakuhitaji kurudia madia ya msingi ikiwa ni pamoja na kurudia uchaguzi. Madai ya Mabadiliko ya Katiba au Katiba ya Wananchi na kudai Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kujiuzulu na Kuundwa kwa Tume ya uchunguzi ni madai yaliyotolewa katika Press Conference ya Tarehe 15/11. Hata hivyo, msisitizo wa awali ni kwa kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi ambayo inaweza kutupelekea kwenye yote hayo. Mtu yeyote asiyemakini kufuatilia mtiririko huo anaweza kupotosha na kusababisha vurugu na uchochezi ambao Chadema, pamoja na jitihada zake za kudai haki zake na za wananchi waliochakachuliwa kura zao inapenda kufuata njia za kistaarabu na za amani. Ni vema yeyote anayetaka kufanya analysis ya hatua za Chadema kwanza akajielimisha vizuri badala ya kuweka hisia zake ( hakuna sababu ya kuandika na mate wakati wino upo, na wakati wowote Chadema tuko tayari kutoa ufafanuzi utakao hitajika, isipokuwa ule unaopaswa kupitia kwenye vyombo vyetu vya maamuzi kama chama cha kidemokrasia.





Eeeeeh Mwaka huu kazi ipo!..shukran Dr.Slaa tumekuelewa sana, lakini natatizwa kitu kimoja tu - Ujumbe huu hasa unamlenga nani? Yaani nani hasa anayeweza kuleta mabadiliko hayo...?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom