Jifunze kupambana nao kama mimi ninavyopambana nawe...utafanikiwa
CCM hawajaacha na kila siku wanazidi kuandika kwenye magazeti yao kuwa chadema ni chama cha wachaga na wakatoliki (kasome ile article ya Antari Sangari). CCM ukiwaacha tu kwenye hii game, wewe ndiye unapoteza.
Mmefanya juhudi gani za kuhakikisha kuwa kuwa hamuwapi leverage wakaweza kuaminiwa na watu kuhusiana na na hayo madai wanayo yasambaza?? Mangapi ambayo mmeyafanya ambayo yamekuwa yakitoa tafsiri ya kuwa wanayoyasema wanapropaganda wa CCM yana chembe za ukweli??? Sihitaji kumention hapa....
Kama ambavyo CUF walivyokosea na kudhani kuwa huo utakuwa mtaji mzuri wa kuhakikisha solid political base nanyi ama kwa kujua ama bila ya kujua mkaingia katika mkenge huo na haswa wakati huu wa kampeni.
Ukiongelea vikofia na kanga katika mikutano ya CUF Pwani wengine wasemaji na mavazi na hata miziki ya maudhui ya kwaya katika mikoa ya Ruvuma, Iringa, Mbeya??? Yote haya ni natural things lakini kama wanasiasa ni lazima ukahakikisha unayacontain ili kulinda na kujenga image ya chama cha wote. No wonder CCM wameamua kung'ang'ania na magwanda, fulana, kanga na kofia za sare ambazo mnakimbilia kudai kuwa wanahongwa lakini ukweli yanaondoa muonekano wa kidini ama kikabila.....
By the way, hizi propaganda za CUF ni chama cha waislam ama mujahidina sio kazi ya wanaCCM tu...hata ninyi mnaamini hivyo na mmekuwa mkipia debe propaganda hizo...umesahau kauli zako hapa na hata hizo picha unazoweka hapa kupambana na hao unao amini kuwa ni CUF???
Lakini zaidi, umesahau kauli ya Freeman Mbowe wakati wa uchaguzi uliopita kuhusu sababu ya kutoshirikiana na CUF???
As I say, CCM huchokonoa...ninyi hutengeneza mazingira ya kushamiri kwa chokochoko zao..............
Unapambana au unaleta udaku tu .. yale yale ya kusema kuwa Zitto anaandamwa na wamachame?
Omar, ulivyokosa msimamo wa nini unataka kufanya kwenye siasa za bongo - kuwa au kutokuwa mpinzani wa mafisadi ya ccm, ulipoteza kila kitu. Siku hizi unabwatuka tu eti unajali sana ndoa za watu ..... kweli? unataka kuongelea ndoa za watu? una hakika hicho ndicho unataka kuongelea, na je utaongelea ndoa za watu zinazomhusisha Kikwete, Zitto, wewe mwenyewe, na wanasiasa karibu wote Tanzania?
kwa vile wewe ni mwanaccm (unayetaka kula pande zote mbili), mtizamo wako utakuwa umepinda tu kwenye hili swala
Nawe unadhani cha kufanya ni huu ukada pofu unao onyesha hapa na ukajipa moyo kuwa ni upambanaji??? Sio ninyi mliokuwa mnajifaragua na kauli mbiu ya MASLAHI YA TAIFA KWANZA...ama kama walivyo CCM kwenu ninyi MASLAHI YA TAIFA ni yale yanayoendana na agenda zenu??
Umesahaua kuhusu ndoa za Mbowe na wengineo pia....bring on
Hata kama tuna mapungufu lakini kamwe kama viongozi hatupaswi kurasimisha ama kuhalalisha mapungufu yetu katika jamii. Lakini zaidi mapungufu yetu hayapaswi kuwa sababu ya kufumbia macho mapungufu mengine wakati tunaamini kuwa hayaendani na maslahi ya taifa ama hao tunaowaongoza ama kutaka kuwaongoza.......
Kwangu mimi nidhamu binafsi ina mahusiano kabisa na nidhamu ya uongozi...............hata kama nashindwa kutimiza hayo
Juzi nilikuomba ukanichukulie kadi yao ili nijiunge mara tu mtakapowashinda na wao kuwa wapinzani....I hope utanifanyia hivyo soon baada ya ushindi wenu adhimu...
Unajikanganya tu bila muelekeo kama kawaida ya mafisadi ya ccm na raisi wao kilaza. Unachoongelea hapa ni nini?
Sikusema nataka kuongelea ndoa, nimekuuliza kama unataka kuongelea ndoa za wanasiasa, Swali langu likawa kuwa, je utaishia kwa Slaa tu au utakwenda zaidi na uongelee Kikwete, ZItto, wewe mwenyewe na wengineo?
Je unafumbia macho ya Kikwete, Zitto, wewe mwenyewe na wengineo? Umeongelea kuhusu ubakaji wa Makamba dhidi ya mtoto wa shule, ni wapi utachora msitari?
Bwa ha ha ha ha ... wanafiki wa ccm bana mnatia aibu hadi basi
Na hizi ndio unaziita hoja zinazotoka kwa vipanga kama wewe.......all the best ili uzigeuze kuwa sera baada ya ushindi wenu adhimu???
Mwafrika;1128932]uchukuliwe kadi mara ngapi? Omar wewe ni mwanaccm, umejaribu jaribu upinzani lakini umeona hakuna pesa na sasa umechagua horse wako kwenye uchaguzi huu (fisadi aliyekubuhu - kikwete).
Misheni yako uliyotumwa ya kuivuruga chadema ilikwama wakati wa uchaguzi wa viongozi wa taifa. Sasa umebaki umechanganyikiwa. Najua inakutia hasira sana kuona chadema ikifanikiwa.
Asante, inafurahisha sana kuwa wanafiki kama wewe hamtakuwepo kwenye sherehe za ushindi.
Duh, Mkuu wangu ama kweli umepoteza kumbukumbu kwani miaka inayoyoma. Mbona 2005 ni majuzi tu Mbowe akigombea urais na JF imekoleza kisawasawa..Bob, hata jamboforums haikuanza kabla ya 2005 labda kama kumbu kumbu zangu sio nzuri
Uliwahi kunichukulia kadi huko kwenu ama CCM??? Hujasema CUF bado maana hamuishi na kuconclusion zenu za kichovu halafu kesho mnawalaumu Usalama wa Taifa kuwa unatoa koclusion za kutunga.....
Hivi kuna anayevuruga CHADEMA zaidi ya Freeman Mbowe????
Ni kweli inaniuma kuona jinsi gani mnafanikiwa kuwauzia watanzania mbuzi kwenye gunia na pia kuona mafashisti waliojivika kilemba cha uanademokrasia kama wewe wanaweza kuwadanganya watanzania eti ukombozi upo mikononi mwao......Just like what Hitler did...
Usiwe na wasiwasi, ntakuja kujumuika nawe katika kilio cha kushindwa.............
Duh, Mkuu wangu ama kweli umepoteza kumbukumbu kwani miaka inayoyoma. Mbona 2005 ni majuzi tu Mbowe akigombea urais na JF imekoleza kisawasawa..
Asante, inafurahisha sana kuwa wanafiki kama wewe hamtakuwepo kwenye sherehe za ushindi.
Sasa hivi hakuna anayeivuruga chadema. Chadema is doing just fine. Chini ya uongozi wa Mbowe,
chadema imeongeza idadi ya wabunge na madiwani nchini na hili linawaumiza sana wanaccm kama wewe.
Unaposema mimi mnafiki, hivi kuna mfano bora wa unafiki zaidi ya huu mnao onyesha hapa JF kwa kucondone mapungufu bwelele ya watu wenu ambayo hayana tofauti na yale ambayo miaka yote hii mmekuwa mkiyapigia kelele...
Kuna wanafiki zaidi ya wale wanao ahidi UWAJIBIKAJIi huku wakifunika usanii wa viongozi wao kwatika matumizi ya fedha za wananchi na hata michango ya kampeni kama ule wa Mzee Sabodo? Kuna unafiki zadi ya ule wa kuhubiri mapambano ya demokrasia huku mkikandamiza na kuwatukana wale wenye mawazo tofauti nanyi??? Kuna unafiki zaidi ya huu wa kuhubiri UADILIFU na FAMILY VALUES huku mkihalalisha/mkirasimisha wizi wa wake za watu....
By the way, ni lini nilikubaliana nawe hata sasa useme mimi ni mnafiki....I am who I am and will never change to suit anybody especially wasanii mbovumbovu kama wewe....
Endelea kujidanganya maana naona huu ni ugonjwa wa wote hata orijinali kopi yenu CCM wanajidanganya kuwa mambo shwari na watapata asilimia 80
Hata mimi naomba na nipo tayari kusaidia hilo maana ni muhimu kwa maendeleo ya demokrasia yetu ya vyama vingi.....