GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Unakuta Ndugu au Rafiki yako kabisa labda amepatwa na Msiba wa Mzazi wake lakini Wewe ambaye pengine kwa sasa anakuona huna Kipato (Pesa) hakutaarifu au unakuja Kusikia kutoka kwa Watu wengine. Na kama haitoshi hapo hapo tena unakuta Ndugu yako kabisa labda anauguza Mzazi wake lakini hakutaarifu ila Ndugu wengine wenye Pesa na Mali wameshataarifiwa.
Hii tabia ya Watanzania (Waswahili) wa Siku hizi imetoka wapi? Ni nani aliyewadanganya Watu kuwa Thamani ya Mwanadamu na Utu wake huwa unapimwa na ama Yeye kuwa na Kazi, Mali na Pesa? Na cha Kukera kama siyo Kusikitisha zaidi ikitokea Mgonjwa amefariki ndiyo utasikia Simu au Meseji ya Kutaarifiwa Msiba.
Kwahiyo unaponitaarifu Mimi kuhusu Msiba wa Mzazi wako unamaanisha kwamba GENTAMYCINE nimeumbwa tu kuja Kuaga Maiti na Kubeba tu Jeneza lake Marehemu ila alipokuwa Mgonjwa sikutakiwa Kuambiwa ili nami basi hata kama sina Hela lakini huenda Dua yangu (Maombi yangu) yangesikika haraka kwa Mwenyezi Mungu kuliko hata hao wenye Pesa uliowathamini?
Na unakuta Rafiki yako mwingine Kafiwa na Mzazi wala hajakuambia ila Wewe Kiustaarabu tu ukampigia Kumpa pole na kumuomba akupe updates za Maziko (Mazishi) anakujibu sawa lakini unaona Kimya na ukijitahidi Kumuuliza huoni Ushirikiano hadi unakata Tamaa ya Kwenda. Na ikitokea asipokuona Msibani baada ya Msiba ataanza Kukupiga Majungu na Kukuona hufai.
Namalizia Kuuliza ni nani aliyewadanganya Waswahili (Watanzania) kuwa thamani ya Mwanadamu ni mpaka tu awe na Pesa, Kazi nzuri pamoja na Mali nyingi? Hivi mnadhani Mwenyezi Mungu alikuwa hajui ni kwanini ametuumba Masikini akina GENTAMYCINE na Matajiri akina Sky Eclat, Bila bila, Chakaza, Mokaze na mama D? Tuache Kudharauliana hapa duniani.