Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 339
- 678
NI MH TUNDU LISU AU CHADEMA WALIO KANYAGA SHERIA?
Na Elius Ndabila
0768239284
Leo John Munyika Katibu wa CHADEMA amewatangazia watanzania kuwa CHADEMA imewafutia Wabunge wanne uanachama. Wabunge hao ni Mh Silinde, Mh Selasini, Mh Komu na Mh Lwakatale huku Wabunge kadhaa wakiambiwa wajieleze.
Wakati kauli hiyo ikijitokeza ambayo inatokana na kile ambacho Mh Munyika amesema ni kukaidi kwa Wabunge hao kukaidi amri ya kuto kuingia Bungeni baada kukubaliana kukaa karantini kwa siku kumi na nne, Mh Silinde amejitokeza na kusema hawakupewa nafasi ya kusikilizwa.
CHADEMA kinao viongozi wengi ambao ni wasomi wazuri wa sheria akiwepo Mh LISU ambaye ni mjumbe wa kamati kuu. Mh LISU anajua kwamba *the right to fair hearing/Audi alteram partem* ni takwa la kisheria. Kuto kuwasikiliza wahalifu ni kwenda kinyume na takwa la katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya CHADEMA.
Je, Mh LISU na Chama hili hawakulizingatia? Wanadhani hawa Wabunge ukimuondoa Selasini aliyetangaza kuachana na CHADEMA baada ya Bunge hili wakienda Mahakamani hawatashinda? Sheria haijazungumza kama mwanachama anaweza kufukuzwa uanachama kiholela, Bali kwa kufuata kanuni na sheria zilizopo. Kwa kuwasaidia CDM wakasome kesi ya James F Gwagilo v AG, High Court of Tanzania at Dodoma, civil case No.23 of 1993 na Said Juma Muslim Shekimweri v AG, High Court of Tanzania at DSM, Miscellaneous civil case no.3 of 1996 iliamuliwa na Samatta J.K.
Ukiondoa hoja ya Mh Ndugai utaona namna CHADEMA walivyokurupuka Kufanya maamzi bila kuangalia sheria za Chama Chao na bila kuzingatia sheria za nchi. Ukisoma Katiba ya CHADEMA ibara ya 6(6.5.6) inasema *"Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatu za kinadhamu bila Kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi"*. Lakini mafu gu yanayofuata yanasema mhusika atatoa utetetezi.
CHADEMA ni Chama ambacho kinatumia jina ambalo halisadifu yaliyomo. Ninadhani walipaswa kufuata sheria walizojiwekea ili waeleweke, lakini kwenda hivyo ni kukurupuka na kusigina sheria.