Ni nani anawajibika endapo vijidudu vya maradhi vinavyofanyiwa utafiti kwenye maabara vikiambukiza binadamu kwa makusudi au kwa bahati mbaya

Ni nani anawajibika endapo vijidudu vya maradhi vinavyofanyiwa utafiti kwenye maabara vikiambukiza binadamu kwa makusudi au kwa bahati mbaya

Nyumisi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
13,499
Reaction score
19,292
Ndugu wana JF, salaam.

Naomba nitoe ushuhuda hapa kwamba wakati nafanya masomo yangu ng'ambo, nilihudhuria semina moja ambayo mtafiti alikuwa anawasilisha mada kuhusu namna anavyoweza kufufua (resurrect) virusi ambavyo vilileta milipuko na kuua mamilioni ya watu miaka mingi huko nyuma na baadaye kutoweka. Katika kufanya hivyo anafuatilia na kuchukua sampuli za mabaki ya binadamu waliokufa kipindi hicho na kutumia hizo sampuli kupata vinasaba (DNA/RNA) vya hao virusi ambazo zitawezesha huo ufufuaji (resurrection).

Katika kuuliza maswali nikabahatika kupata nafasi ya kuuliza swali langu ambalo na wengine waliliunga mkono kwamba haoni kuna hatari kubwa endapo hao virusi waliofufuliwa watapata mwanya wa kupenya na kuambukiza watu. Alichojibu ni kwamba maabara yao inafuata viwango vya juu vya kuzuia hilo kutokea (high biosecurity standards).

Vilevile kuhusu swala la covid mataifa makubwa yameshutumiana kuhusu kutengenezwa kwa hiki kirusi kwenye maabara. Je, kuna namna nchi za kiafrika ambazo mara nyingi ni waathirika wakubwa kuwekeza kwenye maabara za kisasa za kikanda za molecular biology na biotechnology na kuwaendeleza watafiti kwenye hilo eneo kwa ajili ya kijilinda na hawa virusi wanaofufuliwa na kutengezwa maabara endapo wataambukizwa kwa makusudi au kwa bahati mbaya kuliko kutegemea watengenezaji ndo watafute suluhisho?

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom