Ni Nani anayumbisha Serikali, Nani alitoa go ya kumtukana mama, Nani anayetaka Bashe aanguke, Nani anataka biashara K koo isimame?Nani?

Koma kabisa kutuhusisha Wasukuma na failures za huyo malkia wenu wa anga koma kabisaaaaa !!!!!
 
Mimi hapa
 
Kuna namna inatakiwa kupitia sheria za TRA katika utendaji wa kazi zao ,naona kama TRA ipo pale sio kumjenga mfanyabiasha bali kumkamua , ufanyike utafiti wa kina kutoka nchi nyingine wao wanafanyaje , tusijifungie ndani nakutafuta mchawi , Kenya wao mamlaka yao ya mapato inafanyaje kazi ? Pamoja na uchumi wao kuwa juu kuliko wetu

TRA ndo chanzo cha matatizo yote , wao wanachojua ni kukusanya bila kuangalia upande mwingine wa shilingi , biashara chini ya TRA nchi hii nikujitafutia ugonjwa wa moyo na hii ni kwa tz nzima
 
NI CCM MKUU ACHA KUJIZIMA DATA
 
Ukweli umeongea, Kodi inakatwa kwenye nini? TRA watoe formula wao wanakataje... Na Kisha tuwe na mjadala wa pamoja. Mgomo haufanyi chochote kati ya hayo mambo
 
Ukweli umeongea, Kodi inakatwa kwenye nini? TRA watoe formula wao wanakataje... Na Kisha tuwe na mjadala wa pamoja. Mgomo haufanyi chochote kati ya hayo mambo
Shida serikali yako inamazalau , swala apa sio kulaum mgomo swala kero zao zimetaturiwa kwa kiasi gani ? Kama hamna tangu mazungumzo ya awali unataka wafanye nini?

Biashara ni ngum jamani serikali yenyewe inajua ndo maana unaweza ona ata mradi wa mwendo kasi wanashindwa kuendesha , shirika la ndege kila mwaka kuna hasara .

So lazima pawepo na mkakati kuwezesha wafanyabiasha kufanya biashara katika mazingira ambayo wataweza tengeneza faida , walipe kodi na biashara zao ziwe endelevu ili kesho pia wakulipe kodi,

Mfumo mzuri wa kulea wafanyabiashara wa chini kwa ajili ya kesho, n.k

Sasa TRA ya sasa inachojua ni kukusanya tu , na wapo na ubabe wa ajabu , mifumo yao ya kukusanya mapato sio shirikishi,

Swali
Ni bora kuwa na kodi imilivu ili upate walipa kodi wengi wa leo na kesho au kuwa na kodi humivu ili uwe na walipa kodi wachache ambao mda wowote wanaweza funga biashara zao
 
Ukweli umeongea, Kodi inakatwa kwenye nini? TRA watoe formula wao wanakataje... Na Kisha tuwe na mjadala wa pamoja. Mgomo haufanyi chochote kati ya hayo mambo
Mgomo ni njia tu ya anayegoma kupata attention ya kusikilizwa. It's a PROTEST

Tatizo kubwa la serikali ya CCM ni kutokuwa serious na ishu za wananchi wake wakiwemo hawa wafanyabiashara nchi nzima siyo Kariakoo tu

Bado ishu ya kikokotoo. Nakuhakikishia kuwa nayo italipuka tu si muda mrefu

=========================================
By the way, hawa wafanyabiashara si waligoma miezi kadhaa iliyopita?

PM Kassimu Majaliwa alienda mwenyewe kusikiliza kero zao na kutoa ahadi ya kuzitatua. Leo imekuwaje tena?

Kwanini tumlaumu anayelia badala kumtaka kutafuta sababu za kulia kwake maana inawezekana kang'atwa na nge?

Kwa maelezo ya wafanyabiashara hawa, ni kuwa waliahidiwa kusubiri na kwamba matatizo yao yatatuliwa ktk bajeti ya mwaka wa fedha ujao wa 2024/2025 unaoanza July 1, 2024

Wanasema kati ya kero zote hakuna hata Moja iliyofanyiwa kazi na hili liko reflected kwenye bajeti!

Wafanyeje Sasa unadhani?

Jibu ni: PROTEST Ili ku - draw attention ya wahusika kuchukua hatua.

Hii njia inakubalika kikatiba na kisheria!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…