Ningependa kujua kama Nature alikosea au amefanya makusudi.Wasanii dunia nzima hupewa "artists license" ku-deviate toka vitu vya kawaida.
Granted ukiimba Opera au some other "proper" form of art, watu watategemea uwe proper.But the very essence of hip hop, and hence bongoflava, ni rebellion na kutengeneza a sub-culture.Kwa hiyo inawezekana alikuwa anawabeza watu wakuja, inawezekana alikuwa "anaweka msisitizo", inawezekana amekosea kweli lakini ndiyo kioo cha jamii yenyewe, na pengine lugha ya kiswahili ni wakati ikue na ku adapt jinsi watu wanavyoongea na si kuwalazimisha watu kuongea lugha ambayo si hai.
Moreover, kwa kawaida, kama kuna ku-mix li na ri katika kiswahili, watu wa pwani hu default kwenye li wakati watu wa bara hu default kwenye ri, nitashangaa kama Nature, ambaye kwa kadili ninavyofahamu ni mtu wa pwani, amekosea na kuweka ri kwenye li, it will be counter to the norm.
Hata ukiangalia kiingereza cha enzi za Shakepeare, Victoria na Dickens ni tofauti sana na cha sasa hivi, one only has to look at the King James version of the bible and see how obsolete some of the words and spelling have become.Kwa hiyo kama kosa linafanywa na watu wengi vya kutosha linaacha kuwa kosa na kuwa ndiyo standard mpya, watu ndio wanafanya lugha, lugha haifanyi watu.Kiswahili si Esperanto.
Having said that inabidi tujitahidi sana kutumia Kiswahili fasaha na kuondoa makosa yasiyo lazima.