Ni nani hasa mmiliki wa UTT AMIS?

Kwa ni Serikali au watu binafsi?
 
Vipi kuna jambo unalojua, kwamba ni tofauti na what is currently known (hearsay / what is available in public domain) ?
 
UTT AMIS ni Taasisi ya Serikali kwa asilimia 100 na ipo chini ya Wizara ya Fedha. Ilianzishwa baada ya utekelezaji wa Sera za Ubinafsishaji. Baada ya Serikali kubinafsisha mashirika yake katika awamu ya 3 zilipatikana fedha kiasi kadhaa na hivyo serikali ikaona izirejeshe kwa wananchi ili wafaidi matunda ya ubinafsishaji. Hivyo ikaja na mpango huu wa skimu za uwekezaji wa mutual funds baada ya kufanya study nchini India.

Kulikuwa na Mfuko unaojulikana kama Privatization Fund uliokuwa unatumika kuhifadhi fedha za ubinafsishaji, ndipo baadae ikaundwa Unit Trust of Tanzania (UTT) ambapo baada ya kuundwa kama mjumbe mmoja alivyopost ushahidi wa kuundwa kwake hapo juu , Wananchi walitangaziwa kununua vipande (shares) na kukawepo na mpango wa motisha ambapo kwa wakati ule inaanzishwa ulikuwa ukinunu kipande cha shilingi 100 Serikali inakupa shilingi 30 katika kipande hicho. Maana yake kama ulinunua vipande vya 700,000 ulikuwa unahesabika kwamba una vipande vya 1,000,000. Lengo hapo ilikuwa ni kuwafaidisha wananchi wanaowekeza kupata matunda ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma. Baada ya kuuza hivyo vipande ndipo wakaanza kuwekeza kwenye masoko yasiyokuwa na hatari ya kupotea kwa fedha mfano mabenki na benki kuu.

Kama una wasiwasi kwamba UTT AMIS siyo Taasisi ya Serikali unaweza kuverify kwa kwenda UTT ili wakupe documents za usajili, BRELA ambao watakupatia documents za usajili na CMSA ambao ni Mamlaka ya Uangalizi na Usimamizi wa Masoko ya Mitaji, Wizara ya Fedha amabo ni Wizara mama na DSE ambao ni soko la ununuaji na uuzaji wa hisa za makampuni mbalimbali.

Nimeandika haraka ila ninatumaini mtoa mada atakuwa ameelewa. Ila kama kila kitu utataka kuona ushahidi kama tomaso itakuwa ni shida sana.
 
Huyu mzushi Nehemia Kilave kaamka na pombe za jana. Anatupotezea muda tu na MBs zetu
 
Wanaompinga jamaa mimi ni muumini wa β€œwhen you hear hoof beats, think horses, not zebras”, (wanafunzi wa Medical wanafundishwa hilo jambo katika diagnosis)...

Sasa sababu najua jamaa na yeye ana access ya mtandao kama sisi (na ni computer literate ndio maana hata humu anaweza kuanzisha uzi)..., Ndio maana nikasema / nikauliza..., Je anajua kitu tofauti kisichojulikana au wahusika wanachosema ndicho ?
 
WEKEZA UTT ILA KUTOA PESA HIYO UTAKOMA LEO MWEZI SIJAONA CHOCHOTE.KWA KUPOKEA SIMU NI WAGUMU.
UTT NI MR KUKU PRO MAX
Siyo kweli. Sasa hivi kila kitu digital. Unanunua vipande kwenye mobile money platforms na unatoa pesa kupitia same mobile platforms. Kwa Vodacom ni *150*82# halafu unaendelea.

Achana na mambo ya kupiga simu, chukua pesa kiganjani toka UTT
 
Mara paap utasikia zimechotwa na kufanyiwa mambo mengine kama mifuko ya hifadhi ya jamii inavyochotwaga[emoji2]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…