KERO Ni nani huvujisha siri za wateja wa mitandao ya simu?

KERO Ni nani huvujisha siri za wateja wa mitandao ya simu?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

bushagara

Member
Joined
Dec 8, 2012
Posts
39
Reaction score
16
Nimekua nikiona mara kadhaa watu wakilalamika taarifa za mawasiliano yao kwa simu kuvuja, ikiwemo ya sauti, sms na mara nyingine hadi whatsapp.

Nimekua nikijiuliza sana kuwa ni rahisi kiasi gani jambo hili linafanyika kiasi cha kuathiri watu wengi hivi.

Je ni kampuni za simu pekee ndio wanaweza au kuwezesha kufanyika kwa hili? Kama ni wao mbona wanajiharibia biashara? Au kuna chombo/idara/kitengo gani kingine nje ya kampuni za simu kinaweza kuhusika na hili?

Kama kuna watu wamepewa mamlaka haya, mbona kama wanatumia nafasi vibaya?

Tafadhali wenye uzoefu au uelewa na mifano watujuze angalau wanaofanya wajue michezo yao inajulikana na mtu likimpata ajue pa kuanzia.
 
Wanasheria wa wizara wanaosimamia mawasiliano bado wako usingizini , vinginebyo hili wangeisha lifanyia kazi na likasahaulika kitambo sana.
 
Wafanyakazi WASIOWAAMINIFU waliopo kwenye makampuni husika na wale jamaa wa TCRA
 
Back
Top Bottom