Namkumbuka marehemu Cool 9, baunsa wa mabaunsa,
Enzi zile iliaminika kwamba yeye ndo mababe wa Iringa nzima enzi ile,
Japokuwa kulikuwa kuna mtu anaitwa Shetani aliyebarikiwa ambaye bado hakufua dafu kwa Cool 9
Niliishi nae mtaa mmoja Kitanzini Iringa, aliishi nyumba ya pili kutoka kwetu
Nakumbuka mechi ya Lipuli na Simba aliua mbwa mbili za Polisi kwa mpigo
Na polisi wengine walijeruhiwa na kuwahishwa hospitali kama majeruhi
Hivyo baadae polisi walimtumia kusaidia ulinzi wakati wa mechi uwanja wa Samora
Baadae alihamia Mkoa wa Dar es Salaam, pia nilisikia ubabe uliendelea kama kawaida.
Kwa wenye ufahamu zaidi huko Dar watujuze tafadhali.