umenikumbusha miaka ya cool9 iringa nilikuwa niko primary sabasaba,cool9 alikuwa noma pale pote iringa town,nakumbuka mwaka 1994 mdogo wangu aligongwa na gari pale uhindini kwa sadrus na kufa papo hapo,cool9 alikuwepo karibu siku hiyo basi alimchomoa dereva na kumpa kichapo kitakatifu,pia alishawahi kumtemea traffic mate usoni na wala hakufanywa chochote,nimekumbuka mbali sana ingawa naumia sana
Duh Namanyele, hata mimi nimesoma Sabasaba shule ya Msingi enzi hizo.....! Tulihamishwa toke shabaha Agh Khan pale Lugalo.... Baada ya muda kuna wanafunzi waliletwa tokea Azimio nakumbuka kukawa na mikondo miwili A na B.... Pale ndani ya uwanja wa sbasaba kulikuwa na ukumbi wa disco unaitwa Soweto.... Ndo nilipoanzia kumfahamu huyu jamaa anaitwa Kool nine... Kulikuwa na DISCO karibu kila J'mosi kuanzia saa 8 mchana. Na nakumbuka shule tulikuwa tunasoma hata J'mosi mpaka saa 6 mchana.
Na hii group ya wanafunzi iliyohamia tokea Azimio/Ama chemchem ndio iliyoleta mabadiliko ya ajabu pale sabasaba... Nidhamu yoote ikashuka, ikawa mara yangu ya kwanza kuona mwanafunzi anabishana na Mwl na kumkunjia ngumi duh, kukawa na makundi ya kupigana sana kuanzia pale shuleni... Dah umenifanya nivute kumbukumbu za enzi hizo...
Kuna jamaa alikuwa ana mkanda mweusi alikuwa anakaa Gangilonga alikuwa anaitwa Sempaya ..Wengi tulisubiri kuona kama itatokea atapambana na huyu mbabe mwenye nguvu nyingi -Kool nine..... Tulisubiri kwa hamu sana lakini sidhani kama ilitokea..Maana naye ingawa alikuwa mstaarabu alikuwa anaogopewa sana pia - Alikuwa anafundisha makaratee pale Kleruu pia na Mwalimu wa masarakasi Kundya - Pale chuo cha Kreluu.
Huyu Kool nine kufahamika Iringa na sehemu zingine haikuwa kazi rahisi... alipitia vipindi vigumu vya kuwachakaza viongozi wa magroup (Gangstars) mbalimbali pale Iringa... Aliwapa hard blasts mbaya na wakamjua...
Kulikuwa kuna notorious groups maeneo ya kihesa kuna jamaa alikuwa anaitwa Midaku, John Shura, Gerad Njanga, Laiton na kaka yake Juli na wengine wengi sikujui kama wapo hai...Kool nine aliwachakaza woote hawa na wafuasi wao kwa wakati tofauti... na wakamkubali na wakawa wana report kwake....
Huko Kitanzini kulikuwa na akina Sungu na gang lake nao hakuwaacha ..aliwapa mkong'oto wakainua mikono na kuwa wapole kwake....na kuwa marafiki pia bila kupenda.
Kulikuwa kuna mapolisi wakuogopewa enzi hizo .... akina Msangalufu na Mfalingundi (Sijui kama wapo hai) walimjua huyu jamaa wa miraba minne ....Kool nine.....Maana alikuwa anakwenda kuonyesha ubabe wake bar moja ilikuwa inaitwa Mwafrika Kichangani - pale opposite na FFU....
Namanyele nadhani iko siku tutaweka thread ya Iringa sabasaba , gangilonga, kichangani, wilolesi, chemchem kukumbuka enzi hizo.... Nimekumbuka mbaaaali sana sana rafiki yangu..Nimewakumbuka mpaka akina Fire, akina JB Kaduma, Kodo, Mkandawile, hawa jamaa majirani zetu pale Highlands secondary...
Pia nimewakumbuka na baadhi ya waalimu pale sabasaba.. Mh Komba, Mwl Mfiringe, Kasuga, Lupola, Mwinyi kidekeo hilo ni AKA alikuwa nachapa mboko sana, Mgina, sitaki, Mwaitebele, Seme, Simoko, Mandari, Mwl Said, Kuna mwl alikuwa anakunja ndita saaana Mwl Mohamed ha ha ha ha ha ha ha ... Jamani ya kale dhahabu .... (Sijui kama wote wapo hai)
Ila woote hawa walikuwa wanamjua huyu Kool nine .... Alikuwa anakatiza kote bila kizuizi....hata kumbi za starehe walimfahamu na hawakutia neno kwake.
Enzi hizo nilikuwa napita mitaa mbalimbali pale Iringa unakuta watoto wadogo wanajiita Kool nine... Wakimwigiza mambo yake!!! Alikuwa mtu maharufu sana wa wakati wake... (Kama akina Bruce lee, Van dame, Anord...etc)
Huyu jamaa ingekuwa nchi za wenzetu kama USA, UK, France wangemchukua kuwa Actor katika filamu za ubabe, Kwetu hapa Bongo ilikuwa si rahisi kuona vipaji vya watu wa aina yake enzi hizo... Ukweli alikuwa anapendeza sana kuwa ACTOR.
Mungu amurehemu na wengine....waliotangulia kwenye haki..... Duh nimekumbuka mbaaaaliii sana sana. Thanks!