Naona Muro anachukua nafasi ya Zitto sasa,maana kuna kipindi ilikuwa kila ukiamka wakutana na thread ya Zitto,leo hii kila wakati ni 'masredi' tu ya Muro,inakera
wadau nimepita kwa michuzi nikakuta ameweka update za Kova anadai kakamata wengine wawili wataunganishwa na jamaa, kazi kweli kweli, akuponyoka kwa hili sijui, labda tusubiri.
http://issamichuzi.blogspot.com/2010/02/breking-nyuuuuzzzzz-wawili.html#comments
Nasema tena,Achana na polisi + serikali yetu hii, hao unawea kuwaplant tu. Swali ni kuwa Kova na ut uzima wake wote na uzoefu katika jeshi mbona anashuoalia hivi? Kesi gani ambayo ipo katika uchunguzi vielelezo vinawekwa wazi namna hii? Mbona ya Zombe haikuwa transparent kiasi hiki? Toka loni watuhumiwa tunaonyeshwa hadharani katiak press conference kama sio kujishtukia? Na jamaa nao wala hawaogopi wakati tumezoea kuwaona wengine wakijifunika wasimulikwe? kwa nini wengine wa ujambazi huwa wanatuonyesha silaha tu bila watuhumiwa?
Mimi nina wasiwasi na hao watu na Kova mwenyewe kama hatumiwi basi brain yake haijatulia kabisa arudi shule manake mambo mengine hayahitaji kuwa na 3D glasses kuona vizuri kuwa huyu bwana ni mbovu-yale yale ya Mahita
Hivi nyie na akili zenu zote hamuoni kwamba suala hili ni rahisi sana kulitatua?
Je, mmesahau kwamba IGP Mwema (kama sikosei) au DCP Manumba walitamka kwamba "mtandao wa JamboForums" ni wa "kigaidi" na kwamba watuhumiwa Maxence Melo na Mushi waliwekwa hatiani kwa tuhuma hizo?
Jerry Muro hana lolote, hizo rushwa za shilingi 2,000 wanazochukua trafiki ni siri Tanzania? Mbona harushi hewani issue yeyote ya Manji au wezi wengine walio ndani ya CCM!? Inawezekana kabisa kuwa alitaka kumblackmail huyo jamaa wa Bagamoyo!
Waandishi wa uchunguzi wengi wakipata habari ya mtu hupenda kwanza kublackmail...
kwanini ITV walimfukuza Jerry? Jiulizeni kwanza. Ukweli ni kua hakuhama mwenyewe najua wabishi msiojua mtasema alihama. Jerry sio mara yake ya kwanza kula rushwa. Ingawa kwa hili hajakula
Mkuu,
Umesema vyema,na huna sababu ya kuvaa miwani ya mbao.Unachotaka wewe nikujua ninani hasa huyu kijana?Nadhani wako wengi kama wewe walio njia panda hiyo.
Kwa uchache wangu nafahamu kijana huyo JERRY MURO amesoma shule ya Msingi Ubungo National Houses (nyuma ya jengo la RUBADA,opposite na kanisa la KKKT ushilika wa Ubungo).
Nikijana mtanashati toka akiwa shule ya msingi,kama sikosehi wazazi wake waliishi ama wanaishi maeneo ya Ubungo/Mabibo external baada ya kumaliza shule ya msingi akaenda sekondari (sijajua bado ni ipi).alafu amepata mafunzo ya uandishi wa habari either TIME au DSJ kwani hizo shule ziko karibu karibu sana kati ya mwaka 2001 na 2002
nimesoma naye kozi tofauti chuo kikuu, ni rafiki yangu
yeye alisoma 'sociology'
a very determined young person, he had a dream and he wanted to live it (baada ya kupitia rapsha kadhaa za maisha ya kifamilia)
amefanya kazi za utangazaji tangu tukiwa chuoni (alisoma na kufanya kazi part time), ATN, PRT (WAKATI HUO), ITV na saa TBC!!!
Sasa nahisi kupata tabu na elimu, uelewa na dhamira ya kamanda Suleiman Kova, kwa hii staili yake ya kutaka kujisafisha wakati ana haribu kesi. Kama unasema hawa watu ni watuhumiwa kwa nini uwaanike kwa jamii kupitia vyombo vya habari kuwa ni "matapeli sugu" tena kwa kuwapangisha mstari mbele ??? .Kama kulikuwa na rekodi ya CCTV, gwaride la utambulisho la nini tena kwa mtu ambae amewaona watu kwa sura na baadae labda ameonyeshwa kwenye video ya CCTV akiwa polisi??...
Iwapo rushwa haikutolewa au kupokelewa, ya nini kuzungumzia habari ya vitisho wakati mlalamikaji akikwenda kuripoti kuhusu habari ya rushwa ndipo polisi wakaamua kutumia upelelezi njia ya video kuwa nasa watuhumia???...Kama mlalamikaji alijipeleka mwenyewe eneo la tukio kwa minajili ya kutoa rushwa ya mtego lakini hiyo rushwa hakutoa wala swatuhumiwa hawakuipokea, ya nini kusema nguvu ilitumika au utapeli ulifanyika wakati hakua kilichotapeliwa wala madhara kufanyika kwa mlalamikaji?(.....!!)
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni sheria mama ya nchi ipo wazi kuwa mtu anayetuhumia bado ni mtuhumiwa mpaka mahakama yenye mamlaka itakapothibitisha kuwa amehusika katika kosa analotuhumiwa!.
Kama kuna tuhuma zenye uhakika, ya nini kun'gan'gana kuanika kwenye vyombo vya habari hivi kuwa waliokwamtwa ni suga na wamekamatwa kwa njia gani ya upelelezi? Na ni waharifu wangapi wamewahi kuanikwa hivi?..kama jalada limekwenda kwa mwanasheria mkuu au sijui dpp, kwa nini yeye akurupuke kujihami kama sio ana vita binafsi na muro?...hivi kama polisi wana mtambo ya kisasa ya cctv, kwa nini waiitumie kwenye matukio yanayomaliza mali na maisha ya watanzania wengi kama ajali, ujambazi nk waende wakaitumie kwenye tuhuma za rushwa za muro kijana mdogo tu anayepigania maisha kama sio visasi?....
Jerry Muro ni kijana mjasiri sana na ni mkakamavu haogopi mtu namfananisha kwa Tiddo Mhando
Mkuu, kwa kweli Kova asipokuwa macho anaweza kujiabisha vibaya sana kupitia kesi hii na hivyo kushusha umaarufu wake ambao labda alitarajia utapanda. Kama Kova na VIJANA wake wangekuwa makini, wasingekimbilia kuitangaza hii issue kabla mambo hayajakaa sawa. Hivi Kova na vijana wake wanaweza kutwambia ni kwa nini hili suala la mtu kudai rushwa limeshughulikiwa na wao ha hali kuna chombo maalumu cha kushguhulika na masuala ya rushwa (TAKUKURU). Polisi wamechemsha kwani ilikuwa ni mapema mno kumtia Jerry msukosuko wangesubiri kidogo moto wa video zake za polisi na rushwa upoe ndio wamshughulikie.
Tiba
Mwisho wa safari ni Muro au Kova kati yao ataibuka shujaa na tusubiri tuone ni nani kati yao.
Jerry Muro hana lolote, hizo rushwa za shilingi 2,000 wanazochukua trafiki ni siri Tanzania? Mbona harushi hewani issue yeyote ya Manji au wezi wengine walio ndani ya CCM!? Inawezekana kabisa kuwa alitaka kumblackmail huyo jamaa wa Bagamoyo!
Waandishi wa uchunguzi wengi wakipata habari ya mtu hupenda kwanza kublackmail...
jamani wanadamu kwa kukatisha tamaa kijana wa watu ndo ameanza harakati zake you neva know atafikia wapi lakini ndo hivo tena wakubwa wanataka kumfumba mdomo ...
Yale mazagazaga aliyozungumza ni ya alumni wa chuo kikuu? .... mmh! Hivyi vyuo vikuu vya Tz vinatia shaka
Mbona kila mwandishi humu anamtetea Jerry tu?
Dah! Mibongo bwana!