Sasa nahisi kupata tabu na elimu, uelewa na dhamira ya kamanda Suleiman Kova, kwa hii staili yake ya kutaka kujisafisha wakati ana haribu kesi. Kama unasema hawa watu ni watuhumiwa kwa nini uwaanike kwa jamii kupitia vyombo vya habari kuwa ni "matapeli sugu" tena kwa kuwapangisha mstari mbele ??? .Kama kulikuwa na rekodi ya CCTV, gwaride la utambulisho la nini tena kwa mtu ambae amewaona watu kwa sura na baadae labda ameonyeshwa kwenye video ya CCTV akiwa polisi??...
Iwapo rushwa haikutolewa au kupokelewa, ya nini kuzungumzia habari ya vitisho wakati mlalamikaji akikwenda kuripoti kuhusu habari ya rushwa ndipo polisi wakaamua kutumia upelelezi njia ya video kuwa nasa watuhumia???...Kama mlalamikaji alijipeleka mwenyewe eneo la tukio kwa minajili ya kutoa rushwa ya mtego lakini hiyo rushwa hakutoa wala swatuhumiwa hawakuipokea, ya nini kusema nguvu ilitumika au utapeli ulifanyika wakati hakua kilichotapeliwa wala madhara kufanyika kwa mlalamikaji?(.....!!)
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni sheria mama ya nchi ipo wazi kuwa mtu anayetuhumia bado ni mtuhumiwa mpaka mahakama yenye mamlaka itakapothibitisha kuwa amehusika katika kosa analotuhumiwa!.
Kama kuna tuhuma zenye uhakika, ya nini kun'gan'gana kuanika kwenye vyombo vya habari hivi kuwa waliokwamtwa ni suga na wamekamatwa kwa njia gani ya upelelezi? Na ni waharifu wangapi wamewahi kuanikwa hivi?..kama jalada limekwenda kwa mwanasheria mkuu au sijui dpp, kwa nini yeye akurupuke kujihami kama sio ana vita binafsi na muro?...hivi kama polisi wana mtambo ya kisasa ya cctv, kwa nini waiitumie kwenye matukio yanayomaliza mali na maisha ya watanzania wengi kama ajali, ujambazi nk waende wakaitumie kwenye tuhuma za rushwa za muro kijana mdogo tu anayepigania maisha kama sio visasi?....