Ni Nani Kati ya hawa na wengine amefanya physics kuwa ngumu shuleni

Ni Nani Kati ya hawa na wengine amefanya physics kuwa ngumu shuleni

Dah mkuu wapo wengi sana kaka huwezi kuwamaliza wote, ninao wakumbuka fasta fasta ni

Galileo Galilei
Torricelli
Schroedinger
Rutherford
Fermi
Christian Doppler
Bernoulli
Alessandro Volta
Raman
Pascal ( hata watoto wa form one wanamjua)
Fresnel
Compton
Archimedes
Cannon
Kuna m-russia mmoja alikua anaitwa Sakharov, na wengine weeengi sana.
Physics niliiacha advance ila shrondinger ndo nimeuonja ugumu wake maana hata wale tulomajor kwenye chemistry anatuhenyesha
 
Wahuni ninaowakubali
Sir isaac newton
Sir albert eistain
Mr coulomb
 
Physics niliiacha advance ila shrondinger ndo nimeuonja ugumu wake maana hata wale tulomajor kwenye chemistry anatuhenyesha
Hahahaaaa mkuu, kuna Schrödinger yupo kwenye quantum physics, baadhi ya kozi za eng wanamsoma, kuna kitu kinaitwa time dependent na time independent vipo kwenye wave equation, achana navo hivo vitu ni hatari.
 
baba wa physics ni Sir Isac Newton
huyu jamaa kwenye umeme yupo, mechanics yupo, wave motion yupo, electronics yupo, na hesabu yupo, sijui sehemu gani hayupo.

Wanasema ndiye binadam aliyetumia akili yake kuliko hata yesu na mohamad
 
Hahahaaaa mkuu, kuna Schrödinger yupo kwenye quantum physics, baadhi ya kozi za eng wanamsoma, kuna kitu kinaitwa time dependent na time independent vipo kwenye wave equation, achana navo hivo vitu ni hatari.
Basic engineering physics.
 
Wanajamii habari zenu
Ninauhakika kuna wanajukwaa wamewahi kusoma physics ambalo ni two in one yaani literature (laws and define) na mathematics (calculations ),zote hizo zimeundwa na wanasayansi wenye vipaji asilia ili zisomwe na watu wa kawaida je Kati ya hawa Nani alileta vitu complicated (vigumu kupanda)
Isaac Newton
Michael Faraday
Galilei Galileo
Archimedes
Ovagador
Last genius of the century (Albert Einstein)

Daa Me Sir George Simon Ohm alinichanganya sana Umeme Form 5 and 6,
But Kuna Kitabu kinaitwa University Physics aka UP aaah, kudadeki Acha kabisa.
sema ndiyo vile Tena Physics, Mathematics and Chemistry nishasahau.
 
baba wa physics ni Sir Isac Newton
huyu jamaa kwenye umeme yupo, mechanics yupo, wave motion yupo, electronics yupo, na hesabu yupo, sijui sehemu gani hayupo.

Wanasema ndiye binadam aliyetumia akili yake kuliko hata yesu na mohamad
Newton ni hatarii, me namkubali hadi kijana wangu nilimpa jina la Newton alifanana tar ya kuzaliwa kasoro mwezi, na mimi ninavyomkubali Isaac nikampa jina la Newton.
 
Alafu mkuu, hawa wanasayansi sio kwamba ndio wameleta na kufanya vitu viwe vigumu, hawa ndio wamerahisisha mambo hadi leo hii tunauwezo wa kusoma zaidi ya topic tano kwenye kitabu kimoja,

Mfano mdogo chukulia labda kwenye chemistry, ile periodic table kuna element zaidi ya mia, sasa kuisoma tabia ya element moja baada ya nyingine hadi ukazimaliza zote ni ngumu sana, ndio maana kuna wanasayansi wengi walijaribu lakini wakashindwa kuziweka kwenye makundi hadi alipokuja Mendeleev ndio akafanikiwa kuunda hyo PT ambapo wanafunzi saiz wanasoma kwa raha huku wakisikiliza mziki na wengine wakichati, lakini kazi ilikua imeshafanywa na Mendeleev,

Doh!!!kama mwfz anajua anachofanya hawez soma uku anachart otherwise hyo mwfz hajielew
 
Kati ya wanasayansi waliofanya kazi kubwa na ambao hawataweza kusahaulika katika ulimwengu huu in sir Isack Newton, he was the father of classical physics, newtons alitoa laws mbalimbali ambazo ni fundamental katika physics, mfano newtons laws of motion, newtons laws of cooling, newton laws of universal gravitations na nyingine nyingi maarufu zinazosomwa na wanafunzi wa sekondari. Kiujumla Newton alihusika na motion, thermodynamics na gravitation. Kiujumla katika classical mechanics Newton alihusika sana na macrobodies Zaidi! Ndio maana baadhi ya newtons laws Of atractions zinakuwa invalid katika microbodies, mfano katika quantum physics newtons laws zinaongezewa some factors au constants ili kuzipa uhalisia.
Katika morden physics ambayo ipo complicated zaidi ya classical physics kuna vitu kama quantum physics ambayo imeelezewa sana na wanasayansi kama Schrödinger , Dirac, Compton na wengineo ni mueñdelezo wa classical physics, sehemu ambapo sir Isack Newton alifail wao walikuja na njia "solution" mbadala . mfano newton katika newton laws of motion newton hakutoa maelezo yanayojitosheleza kuhusu relativity, na motion in four diamantion pia time dilation " recall the twin paradox" !! Vitu ambavyo vilikuja kuelezewa kinaga ubaga na Einstein laws of ralativity!
Kwa ujumla mordern physics ni ngumu zaidi ya classical physics! Japokua wanasayansi wa morden physics walizitumia shortcomming za classical physics ili kufanya kazi zao ambazo kwa kiasi fulani zilileta mageuzi makubwa katika physics.
 
Wakuu

Kuna muhuni wakuitwa Werner Heisenberg bila huyu Quantum mechanics ingekuwa upuuzi tu
 
Back
Top Bottom