Ni nani Mmiliki Wa Blog Hii Millardayo.com?

Ni nani Mmiliki Wa Blog Hii Millardayo.com?

Sami Misago nae alikuwa anapost after school bash? Fiesta je alipost?
Basi hizi blog zitakua hazina uhuru wa kuamua nini cha kuripoti!
kiuhalisia wamiliki wa hizi blog wanatakiwa wawe free kuripot habari yoyote mbali na vituo walivyoajiriwa
 
Habari Jf

Nimekua nikifuatilia kwa ukaribu sana habari kutoka blog mbalimbali Tanzania, mwisho wa siku nikalizishwa na kuiamini MILLARDAYO.COM kama blog inayocover habari za aina zote ndani na nje ya nchi.

Kilichonifanya kujiuliza, hii blog pendwa ni nani mmiliki wake?

nimejiuliza sana kutokana na ukimya wa blog hii huru kutokuripoti habari za tunza za EATV zilizofanyika usiku wa tarehe 10.

Vipi wakuu, mwenye uelewa wa hii blog inamilikiwa na nani ajaribu kunielekeza.
Pia inasimamia vitu gani hadi iweze kuripoti habari yako kwani kwa tukio la jana ndio lilikua tukio kubwa katika burudani hapa nchini lakini likasusiwa na millardayo kitu ambacho si kawaida yake!

Mwisho, pongezi nyingi ziwafikie East Africa Tv kwa kufanikisha EATV AWARDS 2016
Mmiliki ni Millard Ayo mwenyewe ambaye ni mtangazaji wa Radio na TV Clouds Media.
 
Ni nani humpangia habari za kuripoti kupitia millardayo.com?
Ni yeye mwenyewe anapata habari kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani na nje na baada ya kujiridhisha kuhusu ukweli na uhalali wake inapostiwa kwenye mtandao wake na wafanyakazi wake.
 
Ni yeye mwenyewe anapata habari kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani na nje na baada ya kujiridhisha kuhusu ukweli na uhalali wake inapostiwa kwenye mtandao wake na wafanyakazi wake.
Sawa mkuu!
vp tukio la decemba 10 mlimani city nini kilimkumba hadi akalifumbia macho
 
mleta mada,
siku hizi kuna vyanzo vingi vya kupashana habari...hakuna ulazima kwamba kila habari inayohusiana na masuala ya burudani ilipotiwe na Millard ayo.com.

tayari inaonekana upo well informed kuhusu hizo tuzo,ni kuonyesha kwamba ulipata habari kupitia chanzo kingine.
 
iyo blog ya millard ishakuwa blog ya kureport habari ccm kitambo sana haina tofauti na clouds fm kila cku ccm
 
Sie waswahili hatuna shkrani uyo ayo saalikuwa redio one ndoo hao mawingu wakamjuwa
 
Katika hili Millard Ayo amekosea! Blog yake ni mali yake binasfi haihusiani na mwajiri wake. Anapaswa kutoa taarifa za burudani kama zinavyotokea. Akiendeleza ubaguzi wa namna hii hatafika mbali. Mathalani, akiachana na kituo cha Clouds, hatatangaza habari zinazohusu vituo vingine? huo hautokuwa unafiki? Mbaya zaidi dogo amepitia katika kampuni hiyo ya IPP na ndiyo iliyompa jina town!
 
Kinachonishangaza ni Millard Ayo huyohuyo anayechukuaga vipande vya habari kutoka ITV nakuviweka kwenye blog yake....
Kwahili alilofanya Millard nawashauri ITV wampige marufuku kurusha vipande vya habari zao kwenye blog yake
Akili nyingine bhana, zinazidiwa kufikiri na kuku!
 
Back
Top Bottom