changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Baada ya heka heka za kalenda ya FIFA kwa michezo ya mataifa mbali mbali kuisha, wiki hii ligi kuu Tanzania bara itaendelea tena. Binafsi nilimisi sana soka la timu ya Yanga ya msimu huu hasa likitangazwa na Mpenja.
Nani unautaka, Bangala. Nani unautaka, 'Mwamnyeto.'Nani anautaka 'Aucho dokta wa mpira'. Nani anautaka, 'Kibwana' Nani anautaka, 'Dickson Job.' Nani anautaka 'Feisal.' Nani anautaka 'Yacouba.' Nani anautaka 'Djuma shabani,' nani anautaka Aucho, nani anautaka 'Yacouba.' Nani anautaka, 'Mayele.' Nani anautaka. Yaani zinagongwa pasi za maana na soka safi kabisa.
Wiki hii ni Namungo vs Yanga, natamani kuona kama "nani unautaka" itaendelea hadi huko lindi mbele ya Namungo FC au ndio Yanga itarudi kwenye butu butu? Je, hiyo kama butu butu watarudi na point 3 au ndio wataacha point kadhaa? Na je kama ni mwendelezo wa soka safi je watarudi na point 3 au ndio kufungwa ila chenga twawala?
Tuje upande wa pili, Simba ambao walianza ligi kwa performance mbaya, wiki hii wanarejea uwanjani wakiwa na mabadiliko ya kocha mkuu na kocha wa viungo. Ni mechi yao ya kwanza wakiwa kwenye benchi la Simba. Washabiki wa Simba wanashauku ya kupata mwanga je lile biriani lililokuwa linawanukisha msimu uliopita je Pablo Franco atairejesha? Au ndio limeshindikana kurejea kwavile wapika biriani wamesepa wamebakia wakaanga miogo tu?
Vipi ile hali ambayo ilikuwa hawaipendi ya kufunga tu goli tumoja moja tena kwa tabu itakuwa imeanza kupata muarobaini au ndio yale yale
Yote kwa yote mechi ijayo ya Simba na Ruvu haiwezi kutoa majibu kuhusu uwezo wa kocha mpya kwasababu bado sana kuijenga timu atakavyo lakini kunaweza kutoa kamwanga mwanga hivi kwa mbaali, naam kwa mbali hivi.
Tusubiri tuone je lile soka la Yanga la 'nani anautaka ' litaendelezwa ndani ya lindi na kuendelea kuwa kileleni au kushindwa kufua dafu mbele ya Namungo.
Au point 3 za butu butu?
Vipi na jirani nae anarudi katika soka alilotamba nalo kwa misimu zaidi ya mitatu au ndio hali itakuwa ile kama alivyoianza ligi. Na vipi kuhusu matokei, je watapapasa au watapapaswa.