Sciertist A
New Member
- Aug 4, 2022
- 2
- 0
Chakula, malazi na mavazi ni miongoni mwa mahitaji muhimu ya mwanaadamu kwa karne nyingi, ijapokua karne ya ishirini na moja imekua na ziada ya mahitaji ikiingiza gharama za elimu, afya pamoja na mawasiliano kama ni mahitaji ya mwanadamu yasiyokwepeka. Jee kipato cha mtanzania maskini kinaakisi hayo? Kwenye maisha ya leo ambapo kila mhitimu analalamika kukosa kazi na kila mwenye kazi analalamika kukosa pesa za kumtosheleza ni nani wa kulaumiwa? Tumejaribu kuchambua vipato vya makundi manne kwa ufupi kama ifuatavyo ili kuonesha ni jinsi gani makundi haya yanavyoathirika kwa vipato visivyotosheleza na kwa uhakika bado kuna makundi yamewachwa kutokana na ukomo wa maneno katika andiko hili.
Mhitimu wa Shahada ya Kwanza:
Tanzania ni nchi ambayo inajenga watoto wengi au karibu ya wote kukua kitaaluma na kuwawezesha kwa namna moja ama nyengine kufikia kuwa wataalamu kwenye fani mbali mbali. Hili linaonekana wazi katika sera yake ya elimu bure mpaka kidato cha sita, vile vile katika kusaidia elimu ya juu kupitia mikopo.
Suala la kushindwa kwa wengi wa watoto hawa kuwa wataalamu wa fani ya ndoto yao au kukosa ajira kwa watoto hawa wa kitanzania wanapokua vijana halitajadiliwa hapa, aidha mjadala huu utaeleka kumuangalia mtaalamu aliehitimu shahada ya kwanza na kupata ajira ya serikali, jee kipato chake kinamruhusu kijana huyo kuweza kumtimizia mahitaji yake ya muhimu? Je baada ya kutimiza mahitaji yake hayo anaweza kuwa na ziada ya kuwasaidia wazee wake? Wazee ambao wote wawili hawana mafao ya uzeeni?
Na vipi kuhusu kulipa madeni yaliyomsaidia yeye kufikia kuwa mtaalamu wa fani anayoifanyia kazi leo? Jee kipato chake kinamwezesha kumaliza mikopo ilomfikisha kuwa na utaalamu fulani ndani ya muda mfupi? Lakini pia wakati huo huo kijana huyo amefikia umri wa kuwa na mwenzake na watoto ambao wote ni wategemezi wake, jee kipato chake kinamuwezesha kujitimizia mahitaji yake yote hayo?
Iwapo jibu ni laa basi suali linaelekezwa kwa watengeneza sera jee vipato vinapangwa kwa misingi gani hadi inafikia vijana ambao nchi jana ilitumia rasilimali zake nyingi kuwafundisha watoto hawa leo inawaweka sehemu ambayo wanatupa muda wao mwingi kuitumikia nchi yao kwa kipato ambacho hakiwatoshelezi.
Kipato anachokipokea kijana alieajiriwa serikalini akisha kujitimizia mahitaji yake ya lazima tu kama kula na kodi ya kupangisha nyumba kinakua kimeisha. Kijana huyu kila siku huwa na malalamiko ya kushindwa kuwa na chochote cha ziada cha kuweza kufanya maendeleo mengine yeyote kwa ajili yake na familia yake. Ni nani wa kulaumiwa kwa vipato hivi visivyotosheleza?
Mfanyakazi msaidizi (msafishaji, dereva)
Takwimu za sensa za mwaka 2012 zinaonesha wastani wa kaya moja ya kitanzania inakuwa na watu watano. Fikiria kuna familia moja kama hiyo ya mwanaume mmoja mwenye mke mmoja na watoto watatu ambapo ana kipato cha mwisho wa mwezi tu kilichokua cha uhakika kisichofika hata laki nne akitumie kwa ajili ya kulipia nyumba aliyoikodi kuwanunulia watoto wanaokua kila leo mavazi na kuhakikisha familia yake hiyo hailali na njaa mwezi mzima.
Watoto wake ambao wana ahadi ya kupata elimu bure nchini bado anahitajika kuwahudumia kila leo usafiri wao na gharama nyengine ndogo ndogo za lazima ikijumuisha madaftari, peni na kampasi pamoja na mkoba wa kubebea dhana anazotumia akiwa shuleni.
Vile vile pesa hio hio ndio anayohitajika kuitoa kwenye michango ya familia na pia kutowasahau ndugu na wazee wake alowaacha wakiwa vjijini ambao kila siku wanadhani anaefanya kazi kwenye ofisi ya serikali ni mtu alieshinda maisha na anamwagiwa pesa kila leo katika akaunti yake ya benki. Ni nani wa kulaumiwa kwa kipato hiki?
Wajasiriamali wadogo wadogo.
Kutoka kwenye mfumo wa maisha tulokulia kufundishwa tusome ili tukikua tutakua na ajira, kumetokea waanzilishi wa uoni tofauti ambao unawashajihisha watu kujiajiri wenyewe.
Bado sijafahamu kama uoni huu ulianza baada ya wasomi wengi kukosa ajira ama wengi kati ya wenye ajira kubakia kuwa na hali duni kimaisha na kukawa na umuhimu wa kuwaonesha wanahitajika kupambana zaidi baada ya kupoteza muda mwingi wa maisha yao kujiandaa kuwa waajiriwa.
Baada ya kupambana na mfumo wa elimu uliowekwa na kukwama kuendelea njiani ama kuona ajira uliyonayo inashindwa kukukomboa kuna kijana anaamua kuwa mjasiriamali mdogo, mjasirimali ambae si kama mfanyakazi hana kipato cha kiasi kadhaa mwisho wa mwezi na pengine anahitajika kulipia eneo analofanyia biashara kila leo. Kipato cha mjasiriamali huyo hakiwi na tofauti kubwa na yule anaelipwa kima cha chini cha mshahara na huweza kuwa na maisha karibia sawa na yule wa kima cha chini ama maisha yake yakawa ni ya chini zaidi. Jee ni nani wa kulaumiwa kwa kipato cha mjasiriamali huyu?
Watoa huduma binafsi
Hili ni kundi linalowajumuisha watoa huduma tofauti kama waendesha bodaboda, taxi, daladala pamoja na kutowasahau wabeba mizigo. Ni kundi la muhimu sana kwenye jamii ambalo linachukua jukumu la kuwafikisha wafanyakazi makazini mwao na wasafiri wengine wanakoelekea lakini pia ni watu ambao ukiangalia vipato vyao na kazi ngumu wanazozifanya siku nzima unaamini msemo wa tajiri mkubwa duniani Bill Gates unaosema “Life is not fair, get used to it” unaotafsirika ifuatavyo "Maisha hayana usawa, jizoeshe yalivyo" Kushajihisha watu kuzoea asipofanyiwa sawa sio dhumuni la kuandika andiko hili lakini kukosekana kwa usawa kuna muda unatokana na mifumo ambayo imepangwa kutomfikiria binaadamu mwenzako wakati wa kutengeneza mifumo ama kuandaa sera.
Maoni
Hii ni juhudi ya kufikisha lawama kwa waandaa sera na mifumo ya nchi kuangalia tena mifumo na sera za mzunguko wa pesa ndani ya nchi. Watanzania hawastahiki kuishi maisha duni wanayoyaishi yanayowarejesha nyuma kila leo kusogea kufanya maendeleo yao, lawama ya maisha duni kwa mtanzania linaenda kwa waandaa sera na mifumo basi na hebu tukae chini kuiangalia upya mifumo na sera ili kuwa na Tanzania mpya isiyo na lawama za vipato.

Upvote
0