Mc Justine Mwakibiki
Member
- May 19, 2024
- 14
- 9
Kila Kona ya nchi yetu kumejaa madimbwi, Machozi kila Kona kila chozi linalotoka linaashiria machungu na maumivu, ni nani aliyetayari kukausha madimbwi haya?, ni nani wa kumfuta machozi huyu anaelia Januari mpaka Disemba?, amesahaulika na kila mti nia wa Nchi na hata Mtia nia Jimboni kwake, kila akitaka kujifuta machozi kitambaa chake kinazidi kuloana, ni nani wa kumfuta machozi, na kumuambia sasa IMETOSHA? MWALIMU amelia sana tangu uhuru mpaka sasa bado analia, swali ni hili NI NANI WA KURUDISHA TABASAMU LA MWALIMU?
A)NI YULE ATAKAETENGA WIZARA MAALUMU YA WAALIMU.
Huyu kwa sehemu kubwa ataanza kutibu majeraha ya muda mrefu, kwani wizara hii itakuwa ni chombo muhimu kabisa, kitakachojisimamia chenyewe, kikiwa na malengo ya kumsikiliza mwalimu na kutatua changamoto zake zote, na kikiongozwa na waziri mwalimu ambaye aliwahi kufundisha kabisa, si mwalimu aliyekimbia ualimu na kuutaka ubunge, apatikane waziri mwalimu kabisaa ili awe ndiye mkombozi wa waalimu wenzake, kwakuwa utamu wa ngoma ni kuingia na kuicheza, huyu atakaeunda wizara hii ya waalimu ahakikishe pia CHAMA CHA WAALIMU TANZANIA (CWT), Kinaundwa upya kinakuwa ni chombo huru kabisa kiuendeshaji, kisiwe chama cha waalimu kinachoongozwa/kusimamiwa na serikali, kama kinavyoonekana kwa sasa, wizara hii itatibu kwa sehemu kubwa majeraha ya huyu Mwalimu na kumrudishia tabasamu lake.
B)NI YULE ATAKAEFUTA ADHABU YA VIBOKO, NA KUMWAMBIA MWALIMU WEWE FUNDISHA TU.
Mwalimu anapokuwa chuoni kujifunza masuala ya Ualimu, hufundishwa mbinu mbalimbali za kumfanya mwanafunzi, aelewe kile anachofundishwa, na hata anapoajiriwa na kupangiwa kituo cha kazi, serikali huwa inamuwezesha mwalimu huyu, kwa kumpa vitendea kazi vya kukamilisha kazi yake, kama vile Vitabu vya Kiada/Ziada, Mihutasari mbalimbali ya masomo, Zana mbalimbali za kufundishia n.k, sikuwahi kusikia mwalimu akiletewa fimbo kama sehemu ya vitendea kazi, na hapa ndipo mwalimu akajikuta anakutana na jukumu lingine kabisa ambalo si taaluma yake, ni kweli mwalimu ni mlezi sikatai, lakini tujiulize je hii njia ya viboko ndio njia pekee ya kumuelimisha mtoto?
Na hii imechangia wakati mwingine waalimu kushindwa kutekeleza majukumu yao ya msingi ipasavyo, kwa kutumia muda mwingi kutoa adhabu za viboko badala ya kutumia muda mwingi kuwapa maarifa yao watoto/wanafunzi, Zipo nchi kadhaa hapa Afrika ambazo haziruhusu/zimepiga kabisa marufuku adhabu ya viboko ili kumruhusu, mwalimu kutekeleza majukumu yake ipasavyo, mfano ni nchi ya Misri, na hii inamfanya mwalimu kutia bidii zaidi kitaaluma, ili kumsaidia huyu mwanafunzi kupata maarifa ya kutosha kutoka kwa mwalimu wake, na kwa wale watoto wakorofi ziundwe jela maalumu za kurekebisha tabia zao, tunamtaka kwa dhati huyu atakaeondoa viboko kabisa, ili mwalimu atekeleze jukumu Lake la msingi kulingana na taaluma yake ili awe na tabasamu kwa kazi yake, kama ambavyo Daktari hutekeleza jukumu lake la kitaalamu basi, na kwa mwalimu ikawe hivyo pia.
Nb;picha hii ni kwa msaada wa Google.
C)NI YULE KIONGOZI ATAKAYE WAPELEKA WATOTO WAKE KUSOMA, KWENYE SHULE ZA SERIKALI.
Tunamtaka huyu kiongozi ambaye atakuwa mfano wa kwanza, kupeleka watoto wake wakasome kwenye shule za Umma, kisha baadae akaongoze kutungwa sheria ya kila alie kiongozi wa serikali, ni sharti apeleke wanae wakasome shule za Umma, na sheria hii ikawe ndiyo kigezo cha kwanza, cha kupata teuzi au nyadhifa mbalimbali serikalini, hii kwa namna kubwa itarejesha tabasamu la mwalimu, kwakuwa hakuna kiongozi atakaetaka mwanae apate elimu duni, atapiga kelele waalimu wapandishwe mishahara,madaraja na atatetea vitendea kazi vya ufundishaji viongezwe kwa waalimu, siunajua mkuki ni kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu, kwa maana hiyo tunamuhitaji sana huyu kiongozi atakaekuwa na huu uthubutu yeye binafsi, kisha kuufanya uthubutu huu kuwa ni sheria ili mwalimu akumbukwe kwakuwa watoto wao nao watakuwapo kwenye shule hizo hizo.
D) NI YULE ATAKAETAMBUA THAMANI YA MWALIMU NA KUWEKA KIMA CHA JUU NA CHA CHINI CHA MSHAHARA WA MWALIMU
Ualimu zamani ilikuwa ni taaluma ya heshima sana, nakumbuka kijijini kwetu mwanakijiji alikuwa akiharibikiwa na redio, aliipeleka shuleni kwa mwalimu ili amtengenezee, waalimu wa kipindi kile walifanya kazi kwa moyo, hata kama malipo hayakuwa makubwa lakini ile thamani ya taaluma husika, ilimfanya mwalimu kuipenda kazi yake, Leo hii amekosa mtu anaetambua thamani yake, malimbikizo ya mishahara lukuki anaidai serikali yake, mwalimu hivi sasa mtaani anapewa majina yafuatayo;Mlevi na Mkopaji sugu, kwa kuwa amekata tamaa kabisa, haya yote yamechangiwa na kutotambuliwa kwa thamani yake kabisa, ndiyo maana wakati fulani wale waliofeli kidato cha nne kwa kupata Daraja la 4 ndiyo walipelekwa kusomea Ualimu.
TANZANIA NIITAKAYO MIMI kwa miaka 5 mpaka 25 ijayo, ni ile itakayotupa huyu, atakaerejesha tabasamu la mwalimu, ndiyo maana katika nchi zilizoendelea mfano Marekani na Uingereza mwalimu ndiye anapata malipo mazuri zaidi, hatujachelewa bado.
INAWEZEKANA INAWEZEKANA INAWEZEKANA.

Upvote
2