Ni nchi gani ambayo Marekani imewahi kuwapelekea na kuwalazimisha ushoga?

Ni nchi gani ambayo Marekani imewahi kuwapelekea na kuwalazimisha ushoga?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Kuna wapuuzi wanadhani hatuna akili kama wao. Tunapolalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu, utawala mbovu usiofuata misingi ya sheria, ubadhilifu wa mali za umma, rushwa, utekaji na mauaji ya watanzania wasio na hatia, wanatuambia Marekani na "wazungu" wakishirikiana na baadhi ya watu waliopo ndani ya Tanzania wanataka kutuletea ushoga. Mimi nina maswali kadhaa kwa watu hawa.

Ni nchi gani ambayo inaweza kutupa mfano kwamba Marekani aliivamia au alitumia ushawishi wake akawalazimisha raia wa nchi hiyo wote kuwa mashoga ili tuitumie kama rejea?

Marekani aliipiga silaha za nyuklia Japan hadi akasalimu amri. Toka 1945, Mmarekani ana majeshi yake ndani ya Japan. Umewahi kusikia tuhuma kuwa Marekani amesambaza ushoga Japan?

Mmarekani yupo ndani ya Korea Kusini akiwa na majeshi yake toka enzi za vita ya Korea. Umewahi kusikia tuhuma kuwa Marekani amesambaza ushoga Korea Kusini?

Nimekupa mifano miwili hai ya sehemu ambapo Marekani ana "heavy presence" ya kijeshi. Na hizi ni nchi ambazo zimepiga hatua kubwa za kimaendeleo na ndiyo huko tunaenda kila siku kujifunza na kuwaomba misaada.

Wakati huo huo, hapo Afrika Kusini tu ambapo tunajisifu ushiriki wetu katika kuwapambania kuondoa ubaguzi wa rangi na kuleta usawa, ni moja ya nchi za kwanza duniani kuweka sheria zinazokubali mapenzi na ndoa za jinsia moja.

Hapo Tanzania tunaona wasanii ambao ni moja ya nguzo kuu ya ushawishi wa CCM wakiwa na ukaribu na watu ambao katika jamii yetu wanaonekana na kusemekana ni mashoga (ingawa binafsi siyo mfuasi wa kuhukumu mtu kutokana na muonekano wake lakini ni wazi sheria ingeruhusu kuna uwezekano mkubwa watu hawa wangejitambulisha rasmi).

Nimalizie kwa kusema kuwa mada hii siyo ya kuonyesha mtazamo wangu wala kutoa hukumu kwa mtu yoyote kwenye dhana nzima ya ushoga na maamuzi ya mtu binafsi kuhusu maisha yake. Ninachotaka kufanya ni kuelezea unafki uliopo Tanzania wa baadhi ya watu kutumia hii dhana kama silaha ya kuchafua watu wengine wanaotofautiana nao katika mambo ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom