Nakumbuka wakati wa JK aliwahi kuteuliwa Balozi Siwa kushika nafasi ya ubalozi pale Kigali, PK akamkataa maana anamjua jamaa ni mafia mzuri sana, JK akamwambia kama hamtaki atoe sababu sio unamkataa Balozi bila sababu ambazo zimewekwa kwenye Sheria ya mambo ya kidiplomasia na mabalozi na taratibu zao.
PK hakuwa na sababu za msingi ishu ni kwamba alishazoea kumletea madharau JK sasa akapelekewa kichwa.
Ilimlazimu amkubali maana JK alimwambia kama humtaki na hauna sababu sisi hatuna mwingine wa kumchagua otherwise tufunge uhusiano wa kibalozi. He had no choice, sijui kama alishastaafu mzee.
Hii ndio maana ya kuwa na mabalozi wanaojua ujasusi kumbuka ubalozi una maofisa Hadi wa kijeshi (military attachee) na wengine wengi sana ubalozi sio duka la mangi although siku hizi kuna sehemu unaenda unakuta hawana kazi wanajimwaga mtaani tu nidhamu ya kibalozi hakuna.
Yani unaenda kuna nchi fulani unaulizia information ubalozini jamaa hawana hata msaada wapuuzi wanakula raha tu. Hata ukipata matatizo wao hawana msaada wowote.
Kuna siku nitasimulia kisa cha zamani kidogo kilichonikuta Moscow na balozi hakuwa na msaada kabisa ingali nilipofika nikienda ubalozini kujitambulisha na kuwaeleza purpose ya mimi kuwa kule Hadi appartment yangu. Instead ya kunisaidia ninahitaji kutibiwa nilipata ajali wakati naendesha gari yeye anaishia kulalamika as if yeye ni baba mdogo wangu badala ya kufanya kazi yake.