Mzee Mwanakijiji nadhani mada yako imekujawakati muafaka, sasa hivi ndoa nyingi mtu unalazimika kuoa, sababu kubwa kwa mfano hapa DAR wachumba wengi wanaishi pamoja, au hata kama hawaishi pamoja wanakuwa tayari wanamegana tena bila kujikinga, matokeo yake ni mimba, binti akishapata mimba sasa anakuja na "BABA atasemaje" au MAMA ntamwambia nini lazima tufunge ndoa, au kama ulikuwa umeshatambulishwa ukweni sasa wakwe watakuambia kijana sisi tunataka ndoa hapa, tayari ushampa mimba binti yetu, na wewe labda hukuwa na mpango wa kuoa hapa karibuni, kweli utalazimika kuoa hivyo hivyo tuu au kama ni mgumu basi utabidi usubiri mpaka binti ajifungue ndo uoe, na wengine utakuta bado alikuwa anatafuta na hiyo imetokea sasa binti wa watu kanasa na wewe hukuwa na mpango wa kumuoa yeye, kwa pressure za wazazi wako na wake unabidi sasa uoe, hapo sasa ndani ya NDOA kunakuwa hakuna amani tena. AMBAO hampo kwenye ndoa jamani OA au uolewe na mtu ambaye you cant live without na si you can live with. Mambo hubadirika sana kwenye ndoa, pale ndo maisha ya kweli sasa kama ilizoea kutolewa kila siku sasa mitoko inaweza ikawa once in a month au ikafa kabisa, majukumu yanakuwa mengi hasa mkishapata mtoto, ukiwa na doubt flani ifanyie kazi kabla ya kuji commit, otherwise utakuja lia.