Ni neno gani uliwahi kuambiwa na mpenzi wako likakutouch moyoni na huwezi kulisahau?

Ni neno gani uliwahi kuambiwa na mpenzi wako likakutouch moyoni na huwezi kulisahau?

1.Sitakuacha love,labda uniache wewe (nikimkumbuka hadi chozi linanshuka)
2.I love looking at u all the time,i have finally met my baby's mama'...(biggest liar of all times)

Heheheee athanteee....
 
Sitasahau alikuwa ni X wangu lakini aliugua akanipigia simu halafu akaniambia " mimi ntakufa lakini tambua NAKUPENDA SANA" dah huwa nikikumbuka hadi chozi linasogea kwenye macho maana siku tatu baada ya kuongea nae alifariki kweli.

Poleeee
 
Sito sahau alivyo niambia nitkupnda kwa shida na rha mwanaume mwengine sitamani
wewe ndio chaguo langu, ila mwisho wa siku kawekwa ndani na mtu mwingine nimebaki
kama nilvyo.
 
Nipo na mke wangu mwaka wa 3 sasa
Kuna siku wakati tumekaa chumbani tukawa tunapiga story za hapa na pale mala tukajikuta tunaongelea juu ya familia yao na mke wangu akawa ananiambia juu ya migogoro kadhaa ya kifamilia ambayo ipo kwao Yalikuwa ni maongezi ya kusikitisha sana lakini kilichonigusa sana mimi ni ile kauli yake ya mwisho aliposema nanukuu "ni wewe tu na wanangu ndio mliobakia hapa duniani mnaonipa faraja na furaha ya maisha"
kauli yake hiyo ilijirudia rudia sana kichwani mwangu na tokea siku hiyo niliamua kuacha michepuko yote kwa kutambua kwamba kama kweli mke wangu ananiona hivyo basi kwakweli sitakiwi kuidhihaki hata kidogo imani hii aliyonayo juu yangu
 
Back
Top Bottom