Mwaka 2016 nilienda Tanzania baada ya kukaa muda mrefu US. Rafiki yangu ambaye nilisoma naye Primary alikuwa ndiyo auditor mkubwa pale MSD hivyo bila mimi kujua aliongea na Managing Director kuhusu kupata watu wenye ujuzi na kampuni za kusambaza madawa kama MSD
Wakati na maongezi yao yule rafiki yangu akampa email Lauren Bwanankuru ili aweza kufanya mahojiano ya mwanzo ya nafasi ya Director pale wakati wa likizo yangu Tanzania. Wakati huo nilikuwa nafanya kazi kampuni kubwa ya usambazaji ya US ambayo ipo Ohio Cardinal Health: Healthcare Solutions, Logistics & Supplies. Nikapanga siku ya kwenda kwenye mahojiano ili ikiwekana nifanye kazi pale kama Director.
Baada ya kufika pale huyu Managing Director ambaye naye alikuwa bado ni kijana, tulianza kuongea na kuhojiana:
1. Unarudi lini TZ? Nikamwambia nitarudi nikipata kazi siwezi kuacha kazi na kurudi bila kuwa na uhakika
2. Boss: Natafuta Directors lakini ni mpaka tutume maombi serikalini lakini nimependa sana uzoefu wako
3. Mimi: Asante. Je, Directors wote wako wapi? Siwaoni hapa.
4. Boss: Wamesimamishwa na hii bodi mpya kupisha uchunguzi!
Niliogopa na kuanza kuuliza maswali:
1. Mimi: Sasa nataka nijue boss Je hawa Directors wanaripoti kwako au kwa bodi? Boss akasema kwangu mimi
2. Mimi: Je, Director wanafanya kazi kwa kupitia list ya malengo ya mwaka (company goals). Boss hapana
3. Mimi: Hivyo mtu yeyote wizarani kama mkurugenzi, katibu au waziri anaweza akaja na kumsimamisha kazi Director yeyote ? Boss ndiyo
Nikamwangalia usoni nikamwambia moja kwa moja nakuonea huruma sana. Mimi sitaweza kufanya kazi hapa bila kujali pesa au mafao yenu kwasababu zifuatazo:
1. Kwanza inashangaza viongozi kusimamishwa na bodi wakati wewe hujasimamishwa na wanaripoti kwako
2. Inaelekea ukiwa Director kila mtu ni boss wako na sio wewe pekee. Hii mimi sioni kama ni utaratibu mzuri
3. Usipokuwa na malengo ya kampuni na kila Director kujua majukumu yake ya mwaka ni rahisi sana kwa mtu kuja na kunifukuza bila sababu kwa kutafuta sifa tu. Mimi siwezi kuweka familia yangu kwenye mazingira hayo sina shida ya kazi kiasi hicho.
Aliniangalia na kunishangaa kiasi nilivyokuwa wazi kwake. Nikamwambia kazi yako ngumu na wanavopenda sifa nakushauri utafute wakili mzuri maana sio muda utatengenezewa kesi Boss akacheka! Mimi niko clean.
Niliyosema yote yametokea! Kuna utaratibu mbaya kwenye hizi kampuni na ni ngumu sana kupata watu wazuri kwasababu ya siasa.