Ni ngumu sana kumpata Mwanamke kama Tulia Ackson. Ana uwezo mkubwa, anafaa kuwa Rais

Nashukuruuu Sanaaaa kwa kuliona hilo ambalo wengine tulishaliona tangia muda mrefu sana na kuandika sana humu jukwaani kwa kurudia rudia sana ,katika kueleza uwezo mkubwa wa kiakili na kiuongozi alio nao Mheshimiwa Dkt Tulia Acksoni Mwansasu Dada wa Taifa na Nguli wa sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini.

Bora wewe umejisemea ukweli maana mimi nikiandika naambiwa kuwa namtetea na kumpamba sana. Ok ngoja nisiandike sana leo.
 
Usijipe shida...
Vigezo vya Watanzania kusema mtu fulani ana uwezo mkubwa ni vya kipekee...
 
Shida ninayoona anayo, ni kuna muda anafanyaga mambo kukomoa yani ni kwamba utafanya nini sasa nimefanya.
Hana tofauti sana na ndungai.
Yani kama hakupendi basi atakukomoa hata kama anajua anachofanya si sahihi.
Kama anafanya kukomoa wale anaopingana nao, basi tukubaliane Dr. Tulia ni kiongozi dhaifu, anayeshindwa kujiongoza kihisia ili kukabiliana na wale anaopingana nao kwenye hoja mbalimbali.

Kwanini asiutumie huo uwezo wake wa kujenga hoja mnaosema anao kukabiliana nao, badala ya kutumia nafasi yake kuwaumiza, mimi simkubali kabisa Spika Tulia, hawezi kujiongoza wala hana msimamo, na pale maslahi ya serikali na bunge yanapotakiwa kuwekwa tofauti, hujigeuza mtumishi wa serikali bila aibu.
 
Naunga mkono hoja,

P
 
Mkuu mimi sijawahi mkubali kwa sababu mara nyingi nainaga hayuko fair kuzuia mijadara bungeni kama vile ni mwenyekiti kwenye vikao vya chama.
Nadhani wizara ya sanaa na michezo inamfaa maana anapenda sana kuroll na kupiga picha na wasanii
 
Tulia Kwa profession ni Mwanasheria.

Na Mahali pekee ambapo tulitarajia kuona akionyesha ubobevu na HAKI katika kusimamia Serikali ni BUNGENI.

Ikiwa ameshindwa kujua kitu kidogo tu kuwa Wabunge wasio na chama hawatakiwi kuwa bungeni, atawezaje kuaminiwa position ya juu zaidi?

Mahali panapomfaa Tulia ni DARASANI kufundisha, baas.
 
Mkuu mimi sijawahi mkubali kwa sababu mara nyingi nainaga hayuko fair kuzuia mijadara bungeni kama vile ni mwenyekiti kwenye vikao vya chama.
Nadhani wizara ya sanaa na michezo inamfaa maana anapenda sana kuroll na kupiga picha na wasanii
 
Yaani umeamua kutuchora tutanawazaje au??? Labda sijaelewa nini unamaanisha kaka mtibeli labda utumie muda kunielewesha.... Kwani wewe huwezi kuwa kiongozi wa nchi hiii??? Nakuonaga ukosmart sana ila leo nimekuvua nyota zote aseee
 
Duh aiseee!

Rais mwanamke tena!? Hatuhitaji kitu kama hicho tena baada ya hili kupita
 

Changamoto kubwa ya Tulia ni Uongee aidha kwa hoja au kwa Reference hapo ndipo wengi hushindwa kwa sababu wengi huzungumza vitu kama wapo vijiweni. Porojo.
 
Uwezo unaousema ni huko kuvunja Katiba kwa kuwahifadhi COVID 19 au uwezo wa kutonenepa na kuwa mwembamba milele au kwako wewe uwezo ni kitu gani hasa ?
 
Shida ninayoona anayo, ni kuna muda anafanyaga mambo kukomoa yani ni kwamba utafanya nini sasa nimefanya.
Hana tofauti sana na ndungai.Yani kama hakupendi basi atakukomoa hata kama anajua anachofanya si sahihi.
Siyo kuna muda,inaeleweka wewe nyoosha maelezo kwamba hayo kwenye bold ni hulka ya kike.

Ndiyo maana hata aliyepo sasa akibanwa sana anakaa kimya akidhani anamkomoa mtu kumbe ndiyo anazidi kuvuruga au anakimbilia kusema watu wanamdharau kwa sababu mwanamke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…