Ni ngumu sana kumpata Mwanamke kama Tulia Ackson. Ana uwezo mkubwa, anafaa kuwa Rais

Nimekuwa mfuatiliaji sana wa maandiko Yako ya nyuma. Kwa mara ya kwanza nimegundua unakauchawa si bure, Ukamlinganishe Tulia na Kamala Harris!!! Tulia mwenye jazba za kijinga. Huyu jaribu kumuweka kwenye midahalo na Tundu Lisu uone kitachotokea. Kiingereza ndo umeona akili?
 
Influencer on the 1 & 2 . Kwa wanawake uliokutana nao wewe ambao wapo kwenye siasana.wanaoenakana.sana yaweza kuwa ni.kweli
 
Kwa Hapa Tanzania Wanawake weñye kiwango cha Tulia Akson ni wachache sana


..Dr.Tulia ndiye Spika msomi kuliko wote, lakini huwezi kaniambia ndiye Spika wa viwango kuliko wote.

..Mama Makinda hakuwa msomi kumzidi Dr.Tulia lakini aliongoza Bunge kwa weledi na kumzidi kwa mbali Tulia.
 
Sasa waweke pàmoja Wapewe mdahalo na Tulia Akson alafu utaelewa nazungumzia kitu gani.

Pale bungeni ni wabunge wachache Sana wenye uwezo wa kumpa challenge Kwa hoja huyo Tulia.

..Dr.Tulia ni msomi, lakini mijadala mingine mle bungeni anashida kwasababu ya rungu la Uspika.

..mbunge mwanamke mwenye uwezo, na kipaji cha kujenga hoja, kuwazidi wengine mle Bungeni ni Halima Mdee.
 
Nje ya mdahalo wenye kinga ya madaraka yake ni wa kawaida tu. Inshort hatishi hivyo. Ni kweli ana uwezo fulani, lakini hatishi kwa kiwango unachotaka tuamini.


..tatizo lingine ni namna alivyoingizwa kwenye siasa, na watu waliomuingiza kwenye siasa.

..Tulia angeweza kuwa msaada kwa Watanzania wenzake, kama wale waliomuingiza ktk siasa wangekuwa na mitizamo, au malengo mazuri, na siasa na demokrasia yetu.

..Kulikuwa na jaribio la kumrusha Dr.Tulia toka kuwa Naibu Katibu Mkuu wizara ya Sheria, mpaka kuwa Spika wa Bunge. Jaribio hilo lilifanyika mwaka 2015 lakini wabunge wa Ccm wakalipiga chini.
 
“Kwa mwanaume mwenye upeo mdogo lazima amwone Tulia kama Mjuaji, hasa pale atakaposhindwa kwa Hoja.” Mwanaume mwenye maoni tofauti na yako ana upeo mdogo! Nikukumbushe kuwa tuna Prof. Anna Tibaijuka aliyewahi kuongoza UN HABITAT, Getrude Mongela aliyekuwa mwenyekiti wa mkutano wa UN wa wanawake, na Asha Rose Migiro, kwa uchache. Hao wanawake unaowataka kudai haki zao bila usaidizi mmewapa jukwaa la kufanya hivyo? Huoni manyanyaso wanayopitia baadhi ya wanawake wanaojitokeza kudai haki zao, au za wengine, hasa pale madai hayo napokinzana na matakwa ya watawala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…