MGOGOHALISI
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 4,555
- 6,773
Waziri wa Ardhi Unahujumiwa na watumishi wa idara ya ardhi pale Dodoma Jiji
Imekuwa ni kero kubwa sana kupata control number kwa ajili ya kufanya malipo ya kupata hati kwenye ofisi za jiji Dodoma.
Rafiki zangu wengi wamenunua viwanja Dodoma lakini toka mwezi wa tano wanafuatilia kupata control number ya kulipia ili wapate hati lakini hawajafanikiwa.
Kila wakifika pale wanaambiwa mtandao hakuna. Kwa wanaojua utaratibu wa pale ni kwamba unapoomba kupata hati kwanza unapewa control number ya kulipia sh. 5000 (nadhani hii ni gharama ya maombi japo sina uhakika). Ukishalipia hii kuna control number ya pili inabidi upate ili ukishalipia ndio mamlaka ziandae hati ya kiwanja chako.
Cha ajabu na kushangaza ni kwamba control number ya kulipia 5000 inapatikana kwa haraka bila usumbufu ila ile ya pili ni kama inatoka sayari nyingine
Mbaya zaidi waliofaniiwa kufika kwenye maonyesho ya nanenane eti contol number zilikua zinapatikana lakini inafika leo conrol number hazitoki.
Mpaka naandika hapa ni kwamba watu washasumbuka sana pale ofisi za jiji la Dodoama (Zilipokua ofisi za CDA zamani). Kila siku watu wanaambiwa mtandao hakuna.
Naomba waziri wa ardhi ingilia kati pale ofisi za jiji kuna watu wanatengeneza mazingira ya rushwa waziwazi. Haiwezekani mtu afuatilie control number miezi mitatu eti kila siku mtandao hakuna.
Haiwezekani haiwezeani haiwezekani.