Ni nini athari ya nidhamu mbovu katika cheti?

Ni nini athari ya nidhamu mbovu katika cheti?

Mwanamaji

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
2,905
Reaction score
4,518
Mimi ninasoma stashashada (diploma) ya mifugo katika chuo fulani mkoani Dodoma, mapema mwezi uliopita kulitokea mgomo hapa hali iliyopolekea kufungwa kwa chuo kwa kipindi cha wiki mbili, wakati wa kufungua kila mmoja wa wanachuo alitakiwa Kuja na barua ya mzazi ya Kuomba msamaha kwa kuchochea mgomo. Na pia yalifanyika mahojiano kwa kila mwana chuo ili kuwataja vinara wa mgomo Pamoja na kujaza fomu maalum ya kuahidi kutoshiriki tena katika mgomo.

Jumapili iliyopita tar 28 /06 /2015, kamati ya nidhamu ilikaa na kuwahoji baadhi ya wanachuo ambao NINADHANI walihisiwa kushiriki kwa mstari wa mbele katika mgomo.
Maamuzi yaliyofikiwa na kamati hiyo ni kwamba imetoa adhabu kwa wanachuo wote wanaotarajiwa kuhitimu kua katika vyeti vyao (transcript specifically) kutajazwa nidhamu dhaifu (poor character and attitude to work) hii ni baada ya kukosa vinara wa mgomo hivo wakaamua kutoa adhabu ya jumla.

Naomba kufahamishwa athari za nidhamu mbovu katika cheti changu katika :-
1. Kuendelea na masomo (naweza kunyimwa nafasi nikiomba digrii kwa sababu hiyo?)
2. Katika ajira serikalini au binafsi
3. Athari nyingineyo (taja kama ipo)

Karibuni,

By mwana chuo atakae jaziwa "NIDHAMU DHAIFU " katika cheti chake.
 
Back
Top Bottom