Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Nyakati hizi ni kawaida kumuona kijana wa kiume akiwa amesuka ama kuvaa hereni. Zamani tulikuwa tukiwaona wasanii ndio walikuwa wakivaa hivyo labda lengo likiwa ni kutaka kujitofautisha na wasio wasanii. Lakini bado kulikuwa na maswali ya kujiuliza.
Leo hii ata wasio wasanii, ni kawaida kabisa kumuona kijana wa kiume akiwa na muonekano huo.
Sasa najiuliza, chanzo cha haya yote ni nini, anakuwa na lengo gani? Inawezekana labda wao wanakuwa wanaiga tu bila kujua au wanajua wanacho kimaanisha?
Kukamatika kwa huyu mwanamziki wa huko marekani, kumenipelekea kufikiri zaidi katika chimbuko hili la wanaume kusuka pamoja na kuvaa hereni.
Kwa sababu hii tabia ilianzia kwa wasanii na sisi wengine tukawa tunaiga bila kujua; inawezekana walipokuwa wakishiriki zile sherehe (party), ziliwapelekea wao kutamani kuwa wanawake; ndio maana wakaanza kusuka na kuvaa hereni, wengine kubadili miondoko, kuvaa nguo za kike n.k
Sisi wa huku wa mbali tukajikuta tunaiga mionekano yao bila kujua chimbuko halisi ya hayo mabadiliko.
Bado sijahitimisha tafiti, Karibu tuumize kichwa ni nini chanzo cha kijana wa kiume kusuka ama kuvaa hereni?