Naomba kuuliza hili swali? Ni nini chanzo cha U-Terrorist?
- Kwa nini mambo hayo yanatokea?
- Kwa nini watu wa West na wanaosapoti mambo ya West ndio Target?
- Kwa nini inahusishwa na Uislam na wakati waislam wengi tunaishi nao kwa Amani?
- Kwa nini Mandela alikuwa kwenye Terror watch List?
Kwa sababu sidhani mtu mwenye akili zake anaweza akaamua kuwa tayari kufa kwa ajili tu hampendi mtu fulani na huyo mtu hajamfanyia kitu chochote. Au mtu anayeweza kuuliza vizuri anaweza kuuliza na yule mwenye majibu mazuri anaweza kuyaweka. Kama kumewahi tokea U-terrorist mahali pengine unaweza ukaweka na kutoa sababu ya kwa nini ilikuwa hivyo?
1. mi naamini mambo haya ya ugaidi yanatokea kwasababu watu hao (magaidi) hawakubaliani na hali ilivyo au mambo yanavyoenda.
weusi wakati wako kwenye harakat za kupigania uhuru walikuwa wanaitwa magaidi. walikuwa wanaitwa hivyo na wazungu au vibaraka wao. sisi tuliokuwa upande wao tulikuwa tunawaita wapigania uhuru. mara nyingi naamini hatukupenda kuwaita magaidi. marehemu dk. jonas savimbi tulikuwa tunamuita gaidi (sio sisi wote). kwa wengine walikuwa wanamuita shujaa.
lakini mara nyingine watu humuita gaidi hata wanayemuunga mkono. kwamfano, hata wafuasi wa dk. jonas savimbi wangeweza kukubali kuwa dk. alikuwa anafanya ugaidi kupambana na serikali halali ya angola. na bado wangeweza kumuunga mkono kwa sababu moja au ingine.
lakini wengine wanakuwa magaidi kwasababu ya kushawishiwa au kufuata mkumbo. inawezekana kabisa miongoni mwa wapiganaji wa savimbi kuna waliojiunga kwa kushawishiwa, kwa nguvu, kufuata mkumbo na nk. lakin wakishakuwa kundi moja wote ni magaidi kwetu. mwingine anaweza kuambiwa ukifanya hiki na kile utakuwa umempendezesha mungu. akilishwa maneno hayo kwa muda wa kutosha anaweza fanya hata ujinga mkubwa kabisa
2. kuhusu u-west naona hii ipo kati ya uarabu/uislam na umagharibi (ulaya/amerika) ambao naweza sema ni ukristo zaid. tunaambiwa wayahud (wako na wakristo?) na wapalestina (waislam/waarabu?) wanapigana muda mrefu wakigombea ardhi. na tumekuwa tukipata ripoti za matukio ya kujitoa muhanga (vyombo vya habari vingi ninavyosikia vinaita ugaidi). na tumekuwa tunasikia pia kuwa waarabu au waislam wanaona u-west unaporomosha tradition yao.
kwahiyo naweza sema israel iko karibu zaid na amerika ambayo iko karibu na ulaya. naona ni vita ya ardhi na tradition
3. kuhusu kuhusishwa na uislam hata mi nashangaa. labda baadae, lakin kwasasa mi nna marafik wengi waislam kuliko wakristo. labda wanatuzuga. au waislam wanaohusishwa na ugaid ni wale wenye siasa kaliiiiiiii ambao kusema kweli mi sijakumbana nao. na kama ni magaid, siombei
4. kwa upande wao na maslahi yao na definition yao kipind kile alifit kwenye ugaidi