Ni nini faida ya vyama vya ushirika kwa wakulima Tanzania?

Ni nini faida ya vyama vya ushirika kwa wakulima Tanzania?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Habari wakuu.

Naomba kujua faida za vyama vya ushirika kwa wakulima hapa Tanzania.
 
1. Vyama vya ushirika vinaondoa uwepo wa mifumo holela ya ununuzi wa mazao ya biashara kama Kangomba, Kibubu, Kadumula, Independent farmers, rumbesa, butula, chomachoma na mingineyo.


2. Vyama vya ushirika ni njia pekee ambayo inawaweka wananchi pamoja na kufanya kazi kwa umoja kama jamii moja kutokana na misingi iliyowekwa na waasisi wetu na maadili yake.

3. Vyama vya Ushirika hujenga nidhamu ya utu, umoja, ushirikiano na upendo.

4. Vyama vya Ushirika pia huwezesha kupunguza gharama za uzalishaji pale wakulima wanaponunua pembejeo kwa pamoja. Kupitia ushirika, wanaushirika wanajenga nguvu ya pamoja katika kujadili bei ya mazao yao.

5. Vyama vya Ushirika pia hurahisisha upatikanaji wa takwimu ikiwa ni pamoja na Serikali kupata kodi au ushuru sahihi ikiwa sekta hii itapewa kipaumbele katika ngazi zote.

IMG_20211031_141133.jpg
 
Kweli vyama vya ushirika ni injini ya uchumi pia. Hata hivyo haijapewa kipaumbele kivitendo. Ntarudi. Tuendelee kujadili.
 
... vyama vya ushirika ni miongoni mwa jumuiya za chama! Ni mazalia ya kura za chama chetu; wajinga ndio waliwao.
 
Kweli vyama vya ushirika ni injini ya uchumi pia. Hata hivyo haijapewa kipaumbele kivitendo. Ntarudi. Tuendelee kujadili.
Aliyeuwa spirit ya vyama vya ushirika ni huyo baba wa taifa.akatengeneza vyama fake na kweli vikampa outcome fake.so sad.
 
Back
Top Bottom