1. Vyama vya ushirika vinaondoa uwepo wa mifumo holela ya ununuzi wa mazao ya biashara kama Kangomba, Kibubu, Kadumula, Independent farmers, rumbesa, butula, chomachoma na mingineyo.
2. Vyama vya ushirika ni njia pekee ambayo inawaweka wananchi pamoja na kufanya kazi kwa umoja kama jamii moja kutokana na misingi iliyowekwa na waasisi wetu na maadili yake.
3. Vyama vya Ushirika hujenga nidhamu ya utu, umoja, ushirikiano na upendo.
4. Vyama vya Ushirika pia huwezesha kupunguza gharama za uzalishaji pale wakulima wanaponunua pembejeo kwa pamoja. Kupitia ushirika, wanaushirika wanajenga nguvu ya pamoja katika kujadili bei ya mazao yao.
5. Vyama vya Ushirika pia hurahisisha upatikanaji wa takwimu ikiwa ni pamoja na Serikali kupata kodi au ushuru sahihi ikiwa sekta hii itapewa kipaumbele katika ngazi zote.