Ni nini hasa chanzo cha mgogoro wa mambo ya anga kati ya TZ na KE

iMind

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
3,039
Reaction score
4,889
Sijabahatika kusoma mahali ambapo imedadavuliwa kwa kina kuhusu chanzo cha mgogoro uliosababisha Tanzania kupunguza idadi ya safari za KQ nchini.

Anayejua tafadhali atuhabarishe.
 
Chanzo kikubwa ni kukataliwa kwa Fast Jet kufanya safari zake kuingia Nairobi kutokea Dar,KIA au Zenji.

Hofu ni kuwa shirika la KQ litapata hasara wakiruhusu ushindani wa Fast Jet.

Katika utetezi Kenya inasema mkataba kati ya nchi hizi unaruhusu mashirika ya ndege ya kizalendo na si yakigeni.Fast katika muktadha huu ni shirika la kigeni ingawa limesajiliwa Tanzania.

Tanzania baada ya kuona imebanwa kwa kipengele hicho hapo juu, ikaamua irudi kwenye mkataba na kuibana Kenya kuwa inapaswa ilete ndege kama walivyokubaliana katika mkataba.

Ikumbukwe kuwa mkataba huu uliingiwa wakati ATC ni hai.Hivyo idadi ya safari zilitolewa kwa usawa kati ya ATC na KQ.

Baada ya kuondoka ATC, KQ ikachukua slots za ATC pamoja na kuongeza zingine.Kibiashara hii inakubaliwa.
 
watu wameweka maslahi mbele zaidi kuliko ushirikiano

Source:BONGO NEWSTZ
 
nauliza kwanini serikali ya tanzania wanatumia nguvu kubwa kuitetea fastjet ilhali ni interprise brand ya waingereza? au wamekula rushwa ya fastjet,ndo maana airtanzania inakufa viongoz wanashadadia mataifa mengine
 
nauliza kwanini serikali ya tanzania wanatumia nguvu kubwa kuitetea fastjet ilhali ni interprise brand ya waingereza? au wamekula rushwa ya fastjet,ndo maana airtanzania inakufa viongoz wanashadadia mataifa mengine

Nchi..hii kila kitu kinawezekana...
 
TZ tumelala hatuna lolote tuwezalo, kimsingi hatujitambui !!
 
Kama kenya wali base kwenye mkataba kuikatalia tanzania, basi nao tanzania kufanya reference ya mkataba na kutaka fully implementation ni haki yao ya kimkataba.

UKIJUA HUU WENZIO WANAJUA ULE.
 
Mimi nina suggest tufute kabisa safari za Kenya airways hapa kwetu na tuwatoe wawekezaji wote uchwara kutoka Kenya (Kenya ni ya pili kwa uwekezaji hapa Tz ) maana wamezidi kiburi na kutuburuza
 
Kama kenya wali base kwenye mkataba kuikatalia tanzania, basi nao tanzania kufanya reference ya mkataba na kutaka fully implementation ni haki yao ya kimkataba.

UKIJUA HUU WENZIO WANAJUA ULE.

hawajaikatalia tanzania wameikatalia fast jet, fast jet ipo tanzania lakini ni brand ya waingereza.ingekuwa kampuni ya kizalendo ya tanzania isingekataliwa. hii nchi viongoz wanakula rushwa kupitia migongo ya watu wenye akili za kufata upepo kama wewe bila kufuatilia mambo kiundani na kuchanganua kimoja kimoja. by the way mbona hawa viongoz hawa shadadii air tanzania ambazo ndege zake zote zipo gereji na badala yake wanashadadia fastjet ?
 

Kaka kama kwenye huo mkataba mnaounukuu kukazia hukumu, na sisi tumenukuu ndani ya vipengele vya mkataba huo huo, iwe tulikuwa tunatetea fastjet au vinginevyo hayo yetu ndani, sasa fuateni utaratibu, fungeni midomo.

Mpango upo mbioni tutawaamuru na nyumbu wasije kwenu kenya.

Mahindi mwaka huu mkanunue somalia.

Soon tutaanza zoezi la kusaka wahamiaji haramu, jipangeni.

UKILA NA KIPOFU USIMSHIKE MKONO, imekula kwenu.
 
kwa muda mrefu wakenya wamewafanya watanzania mambumbu ingawa wakati mwingine ni kweli tunaweza kuwa ni mambumbu kwanza hii jumuhiya ni wao ndio waliivunja na walipata faida kubwa baada ya kuivunja mikataba yao mingi wanayoingia na tanzania kwa kiasi kikubwa ni kwa ajili ya faida yao sasa hivi wamejiandaa sisi tunazungumzia sarafu moja wao wameshaingia mkataba na kampuni ya kutengeneza pesa ya ujerumani ili tutakaporuhusu sarafu moja kutumika wao tayari watalazimisha pesa hizo zitengenezwe ndani ya jumhiya huku wakijua kuwa hakuna nchi nyingine yenye kiwanda kama hicho,wametumia sana rasilimali zetu kujitangaza kama vivutio vya utalii vya kwao na pia kitendo cha kuzuia magari ya tanzania kupeleka abiria kwenye airport yao ni cha makusudi umefika wakati na wao wajue na sisi tunaweza kufanya maamuzi kama wao wanayofanya
 
nauliza kwanini serikali ya tanzania wanatumia nguvu kubwa kuitetea fastjet ilhali ni interprise brand ya waingereza? au wamekula rushwa ya fastjet,ndo maana airtanzania inakufa viongoz wanashadadia mataifa mengine

Wewe nawe acha ujinga,tetea taifa lako.Kenya wana udwanzi flani hv na wana hofu na tija inayoonekana mbele kwenye uchumi wa nchi yetu.Kwani KQ inamilikıwa na Wakenya % zote?Fastjet very soon,majority shareholder watakuwa Waswahli.Kuna logıc hapo.Kenya na Rwanda n nchi zenye hulka ya wivu.Kenya tumewapa fursa nyingi za kuwekeza hapa kwetu ikiwemo raia wake wengi kufanya kazi hapa Bongo bila bughudha lakn wao wanapenda sana kuhujumu masilahi ya taifa letu.
 

Wewe n mshamba wa Internation Business.Brand kitu ganı??Brand inaweza kufanyiwa kazi na mtu mwingne.Kwani KQ ınamilikıwa na Wakenya kwa % ngapi?Fastjet inamilikiwa kwa pamoja na Wabongo na biasha sıku hz inaendeshwa hvyo.Kenya wana wivu,walitaka fastjet waende kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…