Ni nini kigetokea kama Shetani asigelikuwepo/Kuasi?

Ni nini kigetokea kama Shetani asigelikuwepo/Kuasi?

Kuna content creator mmoja , Mzungu huwa nimemfollow Instagram. Yeye anaonyesha video za tamaduni za makund ya jamii yaliyojitenga .(isolated) bila interaction ya jamii zingine.

Yaan anaenda ndan ndan huko. Kwa hiyo jamii husika. Anaishi , kula , kutenda na kuvaa kana wao.
Alishawah kuja TZ akaishi na wamasai .

Huko kote anakoenda hakuna Dini.
Hakuna Uislam , ukristo au din yoyote.

Lakin wale watu wanaishi kijamii na mambo yanaenda.
Sasa hawa ukiwaambia habar za dhambi au shetan watakushangaa šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚

Lakin sio kwamba Maugomvi hayatokei, au hawakoseani. Wanafanya yote mabaya na mazur. Bila kuambiwa au bila kuhusisha Shetan na Mungu.
Huyo jamaa kama namjua hivi. Katika content zake anapenda sana za wale watu wanaishi kiuchi uchi sijui watu wa wapi wao ni porini tu muda wote
 
Hajawahi kuhasi, stori za kuambiwa changanya na zako, yaani kuiba ukaibe wewe useme ni shetani tu. Ngastuka, popo mbili zavuka mto, macho!!!!... usiwe kama kipofu. Stori za Mungu na shętani ni hadith za sungura na fisi. connect the dots.
Sisi tunasoma kilichoandikwa mkuu
 
Haiwezekani asiwepo. Dini ni majukwaa yanayotumika kumulika asili yetu, na asili yetu inahusisha mpambano wa mema na mabaya pasipo mwisho.

Shetani anawakilisha mabaya. Shetani ni ishara tu. Dini zote zina upande wa mazuri, na wa mabaya.
Sijakuelewa unaposema haiwezekani asiwepo ili hali tunasoma tunaona alikuwa mwema(hakuwepo) ila badae alipoasi ndo akawepo sasa.
Vipi angeendelea kuwa mwema hadi leo?
Ndo msingi wa swali langu mkuu
 
Hajawahi kuhasi, stori za kuambiwa changanya na zako, yaani kuiba ukaibe wewe useme ni shetani tu. Ngastuka, popo mbili zavuka mto, macho!!!!... usiwe kama kipofu. Stori za Mungu na shętani ni hadith za sungura na fisi. connect the dots.
šŸ’Æ
 
Dah, Haya bana.
Ila mm najua ww haumini Mungu kama yuko. Kwahiyo hauwez muamin Shetan pia.

Turud kwenye hoja ya mtoa Mada.
Kama shetan awepo au asiwepo hawez badili namna Binadam tunavyoishi.

Yaan hata bila kiumbe kinachoitwa Shetani, binadamu bado ana tamaa, hasira, na ubinafsi. Kwahiyo Migogoro inaweza bado kuwepo kutokana na ushindani wa rasilimali mfano chakula, ardhi, madaraka, ugomvi kama ilivyo kwa wanyama wengne.

Kwahiyo hiki ndio kingetokea/kinachot
okea. šŸ‘†šŸ‘†šŸ‘†šŸ‘†
Kama ni hivyo ni wazi shetani hakubadili kitu chochote kimsingi anasingiziwa?
 
Nikama nafumbuka macho. Mungu naamini yupo, ila shetani sina uhakika kama yupo. Maana utaambiwa MUNGU anapenda mema, ukifanya kitendo kisichokubalika na jamii, utaambiwa we ni shetani au una shetani. Inamaana MUNGU hamuoini shetani?
Ambwene Mwasongwe anakuambia tusingejua mtu mrefu kama iwapo huyo mtu mfupi asingekuwepo.

Au tusingemjua mtu mweupe iwapo website wasingekuwepo.

Hii ina maana kwamba uwepo wa shetani moja kwa moja una tambulisja uwepo wa Mungu. Swali langu linabaki kuhoji imagine shetani asingekuwepo kabisa inamaana kingetokea nini?
Dini zingekuwepo? Kwa kazi gani?
 
Hajawahi kuhasi, stori za kuambiwa changanya na zako, yaani kuiba ukaibe wewe useme ni shetani tu. Ngastuka, popo mbili zavuka mto, macho!!!!... usiwe kama kipofu. Stori za Mungu na shętani ni hadith za sungura na fisi. connect the dots.
'Kuhasi' tena na si 'kuasi'!

Mkuu missunderstanding hizi msizozijali zinawashushia hadhi sana.

Mantiki unayo nzuri sana katika comment hii, lakini kukanganya sarufi katika uandishi wako kunashusha thamani ya 'madini' uliyoyaleta 'sokoni'.
 
Tuendelele kuvumiliana wakuu.

Hoja yangu ina mashiko hvyo naomba nisikilizwe.

Ukisoma kitabu flani cha wasabato kinachoitwa Great controversy (Between {God}Christ and Satan )

Au kwa jina jepesi kinaitwa PAMBANO KUU (KATI YA WEMA NA UBAYA) cha Ellen G White.

Kitabu hiki kinasema Shetani ni muasi tangu mwanzo,kinasema shetani ndio baba wa ubaya wote hapa Duniani nk

Swali linakuja iwapo basi shetani asingelikuwepo kabisa Au asingeliasi huko mbinguni je nikweli kwamba Tungekuwa tunaishi bila magonjwa yoyote? Nikweli tungeishi pasipo kufa ,wivu wala kuzini kabisa?

Je kuna raha gani ya kuishi uchi wewe na watoto wako au bado akili zetu zingekuwa kama wanyama?

Kumaanisha hata Gari,simu ndege,meli ,Tren na ujenzi wa nyumba nzuri usingelikuwepo.

kwa mtazamo wako hii dunia ingefaa ikiwa agizo la mungu bado ni lilelile enedeni (mkazaliane) mkaijaze nchi?

Kwa upande wangu sielewi na sina majawabu kwakweli.
Chukua mfano kwa wahdzabe
 
Thing comes in pairs,..Magharobi na Mashariki. Usiku na mchana, kupendwa na kuchukiwa. Dume na jike. Same kwa Mungu na shetani.
 
Sijakuelewa unaposema haiwezekani asiwepo ili hali tunasoma tunaona alikuwa mwema(hakuwepo) ila badae alipoasi ndo akawepo sasa.
Vipi angeendelea kuwa mwema hadi leo?
Ndo msingi wa swali langu mkuu
Shetani yupo kwenye hadithi na sio uhalisia!

Wahusika wa hadithi humulika tabia za watunzi wao. Mungu na shetani wanamulika tabia za watunzi wao ambao ni binadamu.

Kile kisa cha shetani kutupwa mbinguni ni mtindo tu wa simulizi uliotumika kumtambulisha.

Ili shetani asiwepo, inabidi binadamu asiwe na ufahamu wowote kuhusu mabaya. Hii haiwezekani, ndo maana kila dini ina upande wa mwanga, na wa giza.
 
Back
Top Bottom