May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Kwa miaka ya karibuni kumeibuka Kampuni kadhaa zinazojihusisha na uuzaji wa Viwanja kwa njia ambayo wanamruhusu Mnunuaji kulipia kwa awamu au kidogokidogo.
Wengi watakwambia ulipe kiasi fulani mwanzo kisha utaendelea kulipia kiwango kilichobaki ndani ya miezi sita au mwaka au kwa makubaliano mtakayojiwekea.
Ambacho sijawahi kusikia kutoka kwenye Kampuni hizi ni nini kitatokea iwapo Mnunuzi atashindwa kumalizia malipo au kuchelewesha kupita kiasi.
Na je ni kwa nini Wakopeshaji hawa wasiweke wazi kwenye matangazo yao kile watakachokifanya iwapo Mtu atashindwa kumaliza kulipa, kama ni kupelekana kwenye vyombo vya kisheria, kunyang'anywa hicho Kiwanja, au iwapo watarudisha pesa uliyokwisha walipa na haikutimia?.