Noel Ngiama Makanda
JF-Expert Member
- Oct 14, 2018
- 1,782
- 3,111
Leo nimewiwa niandike machache kuhusu hili janga la COVID-19. Ni ukweli usiopingika kwamba huu ugonjwa umelipuka kukiwa hakuna maandalizi makubwa ya kukabiliana nao duniani. Mambo mengi hayajulikani na hata jinsi ya kukabiliana nao bado ni mtihani mkubwa.
Nchi nyingi duniani zimeanza kupata matokeo chanya ya mapambano dhidi ya COVID-19. Ingawa kuna wasiwasi kuhusu second wave ya ugonjwa huu, hasa hasa ukizingatia kuondolewa au kupunguzwa kwa vikwazo vilivyoleta hayo matokeo chanya. Gharama za kiuchumi zimesababisha nchi nyingi kulegeza au kuondoa restrictions.
Wengi tupo nyumbani tukisubiria kupungua kwa maambukizi. Biashara zetu na kazi zetu zinategemea kupungua kwa maambukizi. Nchi nyingi zimekuwa zikitoa timeframe ya hizo restrictions, kiasi kwamba unaweza kuplan hata what next. Na hata restrictions zao nyingi huwa zinategemeana na data(idadi na trend ya maambukizi na vifo, uwepo wa vifaa tiba,na athari za kiuchumi). Miongozo na mipango mingi inapatikana kwenye websites za serikali. Kwa Tanzania sijasikia kuhusu timeframe ya hizo restrictions na websites za serikali zinakuwa na vitu vichache kutusaidia sisi tuweze kuplan vizuri. Mfano mdogo ni hatujui ni lini wanafunzi watarudi shule.
Kwa Afrika ya Mashariki, kumekuwa na taarifa nyingi zikionyesha uwepo wa maambukizi mengi maeneo ya mipakani. Nchi jirani(Zambia, Uganda, na Kenya) zina-report wengi wanaokutwa na maambukizi ni madereva kutoka Tanzania. Tunajua wataalamu wetu wa afya wanafanya kazi nzuri sana kupambana na ugonjwa huu, lakini hatuelewi(sielewi) kuhusu wataalamu wa sera na mipango wanachokifanya.
Ukiniuliza kuhusu Rwanda au Kenya, ntakuelezea kuhusu baadhi ya hatua walizochukua, na hata end game au ultimate goals zao zinajulikana. Malengo na mipango inatakiwa iwe SMART(Specific, Measurable, Achievable/Attainable, Relevant and Time-Based). Inabidi uweze kupima kama mipango yako inafanya kazi kwa kutegemeana na indicators ulizojiwekea( numbero of deaths au new infections), na inabidi uweke timeframe ya hiyo mipango yako. Kwetu sisi ni haileweki kama ni taarifa hakuna au mipango ndio hakuna.
Mwisho kabisa, napenda nitoe rai kwa wataalamu wetu na watunga sera wetu. Inawezekana hatuwaelewi kwa sababu hamtuelezi mnachokifanya. Inawezekana hatuwasapoti kwa sababu mpo kimya. Tuelezeni nini cha kufanya kwenye kipindi hiki kigumu. Ingependeza kama kungekuwa na team inayotuelezea wananchi kuhusu mafanikio na changamoto kwa ratiba maalumu. Watanzania ni wazalendo kweli kweli, ni rahisi sana kupata support yao ukitumia approach sahihi.