Ni nini sababu ya kupungua kwa mikopo ya HESLB mwaka 2021?

Ni nini sababu ya kupungua kwa mikopo ya HESLB mwaka 2021?

Benno Bongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2017
Posts
620
Reaction score
704
Tatizo hasa ni nini kupungua kwa mikopo 2021 na watu wengi hususani wanaotoka kaya maskini kupata chini ya asilimia 50.

Karibu tujadiliane
 
Tujadili nini sasa na washika rungu wameshafanya yao.

Tafsiri ya bodi ya mikopo ni nini?

1. Si lazima wote muwe madaktari
2. Madaktari wamejaa mitaani
3. Afya ni ualimu uliochangamka kwa hivi sasa
4. Afya sio kipaumbele tena unakosa mkopo kama anavyoweza kukosa mkopo mwanafunzi anayesomea ususi na ufinyazi
5. Serikali haina sehemu ya kuwapeleka madaktari hivi sasa

Kwanini nimelenga afya zaidi hapo juu dhidi ya bodi ya mikopo

1. Afya ndo kozi pekee ambazo ukikosa mkopo hasa mtoto wa masikini unayo 90% yakutoenda chuo sababu ada zake ni kubwa mno.

ASANTE
 
Tujadili nini sasa na washika rungu wameshafanya yao.

Tafsiri ya bodi ya mikopo ni nini?

1.si lazima wote muwe madaktari
2.madaktari wamejaa mitaani
3.afya ni ualimu uliochangamka kwa hivi sasa
4.afya sio kipaumbele tena unakosa mkopo kama anavyoweza kukosa mkopo mwanafunzi anayesomea ususi na ufinyazi
5.serikali haina sehemu ya kuwapeleka madaktari hivi sasa

Kwanini nimelenga afya zaidi hapo juu dhidi ya bodi ya mikopo

1.afya ndo kozi pekee ambazo ukikosa mkopo hasa mtoto wa masikini unayo 90% yakutoenda chuo sababu ada zake ni kubwa mno.

ASANTE
wewe waliokuzoesha afya lazima upate mkopo ndiyo hao hao wanaokuzoesha kuwa afya siyo lazima upate mkopo. Labda kama kuna sheria katika hili!!!
 
Una maana gani unaposema "kaya masikini"? According to bodi ya mikopo,kaya masikini Ni wale wanaosaidiwa na TASAF.Hao wamepewa mkopo 100%.Wewe Kama kaya yako sio dependant wa TASAF huna vigezo vya kuitwa kaya masikini.
 
Mm nilipata asilimi chache na vyeti vya vifo wazazi niliambatinisha, jambo la msingi ni kupambana tu na kama mapambano huyawezi basi unakaa kando tuu
Umepata % ngapi mkuu?
 
Una maana gani unaposema "kaya masikini"? According to bodi ya mikopo,kaya masikini Ni wale wanaosaidiwa na TASAF.Hao wamepewa mkopo 100%.Wewe Kama kaya yako sio dependant wa TASAF huna vigezo vya kuitwa kaya masikini.
unajua vigezo vya mtu kuingia kwenye programe ya Tasaf jinsi kulivyo na urasimu? bodi ya mikopo yenyewe imetangaza wanaofadhiliwa na Tasaf ni wanafunzi 782 pekee tanzania nzima! je unaamini kaya maskini tanzania ni za hao wanafunzi 782 tu nje ya wanafunzi zaidi ya laki moja
 
Kukosa mkopo ni malalamiko, na kulipa tena deni ni malalamikooooo.

Mbongo na malalamiko ni pete na kidole
kulalamika watu wengi walikuwa wanalalamika ile increament ya asilimia 6 kila mwaka nje ya riba ambapo inakulazimu ulipe deni la mkopo mpaka unastaafu tofauti hata na mikopo ya benki ya kufanyia biashara sembuse huu wa elimu
 
kama hivi ndio kwenda mbele basi ndio wameharibu kabisa
muda wa vikao unakuta mtanzania mwenzetu kashashiba nyama za kutosha kashushia na sharubati basi anasahau kabisa matatizo ya wengine.
 
Back
Top Bottom