Ni nini sababu za viongozi na wananchi wengi kujitokeza kuchukua fomu za kugombea ubunge?

Ni nini sababu za viongozi na wananchi wengi kujitokeza kuchukua fomu za kugombea ubunge?

Revolution

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2008
Posts
1,436
Reaction score
1,769
Kipenga kimepulizwa jana tu ila wimbi la uchukuaji wa fomu za kugombea ubunge na udiwani ni wa kiwango cha kasi sana! Ni haki ya kila mtanzania kikatiba kuwania nafasi za uongozi wa kisiasa. Lakini ninachojiuliza mbona kipindi hiki watu wengi wana shauku kubwa sana ya kuwania nafasi hizo? Jibu ninalolipata ni kwamba pamoja na kiu ya watia nia kutaka kuwawakilisha wananchi katika muhimili wa bunge lakini inaelekea kazi hii inalipa sana na ndio maana watu waapigana vikumbo (na hapo bado mchujo haujaanza).

Wito wangu ninaishauri Serikali yangu sikivu iboreshe mazingira ya mihimili mingine kama Mahakama na Serikali (Executive) kwa kuwa sasa hadi wakuu wa mikoa na Wakuu wa Taasisi wanaukimbia uongozi wao na kujitosa kwenye ubunge.

Ninajua Serikali yetu ni sikivu na itafanya jambo! Au kama kuboresha huko kwingine hakuwezekani basi ipunguze mishahara na marupurupu ya wabunge ili angalau kuwe na usawa hata kama sio wa 50/50 ila tofauti isiwe kubwa kwa kiasi kikubwa. Hii Nchi ni yetu sote na pia wote Serikalini tunawatumikia wananchi.
 
Haya ndio mambo niliyokuwa ninayaongelea. Ubunge unakimbiliwa na Wakuu wa Mikoa.
 

Attachments

  • VID-20250701-WA0075.mp4
    10 MB
Back
Top Bottom