Ni nini suruhisho/tiba ya hasira

Ni nini suruhisho/tiba ya hasira

Promenthous

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2013
Posts
338
Reaction score
397
Habari zenu wadau, naishi na mwanamke ambae nimezaa nae mtoto mmoja, sasa anamiaka miwili, tatizo la huyu mzazi mwenzangu anahasira sana kiasi cha kushindwa kuzicontrol.

Kuna wakati aligombana na majirani zake alitishia kuwachoma kisu,nampango wa kubariki nae ndoa lakini nikifikilia swala la hasira zake nakata tamaa

Je, nini suruhisho ya hilo tatizo lake, naomba ushauri wenu.
 
mtihani sana huo maisha magumu sana hayo na habadiliki huyo ng'o!
 
Hakikisha "unamkaza" vizuri...hiyo ndio dawa ya wanawake wa hivyo...
 
Ndo usimvuruge sasa, kwani anakasirikaga bila sababu?

Sababu zinakuwepo,lkn yy akikasilika anakuwa kama mbogo,anaweza kufanya chochote na mwisho uishia kuregret tu,yn huwa hawezi kuzicontrol hasira zake.
 
Sababu zinakuwepo,lkn yy akikasilika anakuwa kama mbogo,anaweza kufanya chochote na mwisho uishia kuregret tu,yn huwa hawezi kuzicontrol hasira zake.
watu kama hao sijui wanasaidika vipi,kuna mshikaji wangu ana hasira kama hizo,ukimkasirisha anaweza kukupiga na lolote alichonacho hata panga halafu anajutia baadaye,alimpiga mtu jiwe la kichwa akafa pale pale now yupo jela kafungwa 20 yrs
 
Utamfanya jamaa asibariki ndoa bure
 
watu kama hao sijui wanasaidika vipi,kuna mshikaji wangu ana hasira kama hizo,ukimkasirisha anaweza kukupiga na lolote alichonacho hata panga halafu anajutia baadaye,alimpiga mtu jiwe la kichwa akafa pale pale now yupo jela kafungwa 20 yrs

Duh,hatari,nakumbuka kunawakati tulizinguana akanirushia chupa,bahati nzuri niliikwepa,sasa ananitia mashaka na hizo hasira za kijinga.
 
Hakuna mwanamke amabae hana hasira tena umesahau huwa na maneno mengi sana mengi ya hayo maneno ni ya kuudhi so inabidi umchukulie poa tu na kumsamehe
 
Habari zenu wadau,naishi na mwanamke ambae nimezaa nae mtoto mmoja,sasa anamiaka miwili,tatizo la huyu mzazi mwenzangu anahasira sana kiasi cha kushindwa kuzicontrol,kunawakati aligombana na majirani zake alitishia kuwachoma kisu,nampango wa kubariki nae ndoa lkn nikifikilia swala la hasira zake nakata tamaa,je nn suruhisho ya hilo tatizo lake,naomba ushauri wenu.
pole ndugu.
Kuna principle inaitwa count to ten Mwambie aitumie hakika itamsaidia.
Mwambie kila wakati anapokutana na jambo linaloamsha hasira zake ahesabu one to ten kabla hajafanya maamuzi yoyote then ndo afanye. Ikiwa kwa maneno ama vitendo.
Nilikuaga nahasira hadi natetemeka lakini baada ya kuanza kutumia njia hii niko sawa tu. Mwambie shemeji aitumie afu utatupa mrejesho.
 
mi nina hilo tatizo ni mwanaume mmoja tu kaliwezea ambae sina statment mbili mbele yake kwa kifupi natamani anioe hata kesho kanifanya niwe mpole mpakanmaragiki wamenishanga

NIKUAMBIE KAFANYAJE
 
Back
Top Bottom