Tatizo lako unaiangalia katiba kwa jicho la CHADEMA ukidhani CHADEMA itakuwepo miaka yote, ukijadili katiba angalia vizazi vijavyo, maana unachokidharau Leo utakuja kukihitaji kesho. Jadili katiba kwa kuangalia manufaa sio CHADEMA.
Kuhusu Kenya, uchaguzi ulikuwa mgumu, waliachana kwa tofauti ya kura laki mbili, Sasa kura laki mbili ni eneo moja la bungoma huko magharibi ndio zilimpatia Ruto ushindi, Sasa unaweza kudispute hizo kura na Uchaguzi ukaenguliwa. Kenya wapo mbali usimuangilie odinga, Kuna vizazi vinakuja vitahitaji kupinga matokeo wakati odinga hayupo.
Nakushauri, unapojadili suala la Katiba usiingize vyama au personalities utaharibu, Bali angalia mambo ya manufaa yanayohitajoka kwenye katiba. Kwa mfano katiba yetu Ina mahakama ya katiba Constitutional Court, lakini hiyo mahakama haijawahi kufanya kazi kwa sababu haitoi locus standi na procedures za kufungua mashauri kwenye hiyo mahakama. Hivyo unaweza kupendekeza katiba mpya iweke hayo mambo muhimu kwenye mahakama ya katiba, lakini kuanza kudai CHADEMA haitashika madaraka au odinga nk, haitasaidia.