LD
JF-Expert Member
- Aug 19, 2010
- 3,014
- 578
Je, tukisema Ladies wanapenda wawe treated kama Baby Girls ni sahihi?
Naweza kusema ni sahihi, kutokana na vile pia moyo wa mwanamke ulivyoumbwa. Na kama wanaume wangekuwa wanafanya hayo hakuna mwanamke ambaye angekosa uaminifu, kwa sababu mwanamke pia ameumbiwa kuridhika na upendo wa mtu mmoja.
Biblia inasema enyi waume wapendeni wake zenu, ina maana utii wa mwanamke kwa mwanaume inategemeana na jinsi anavyopendwa. Kumbuka upendo una nguvu, kwa hiyo upendo unanivuta mimi mwanamke kukutii wewe mwanaume.
Nina imani kama wanaume wangekuwa wanawapenda wake zao kwa jinsi hiyo kusingekuwa na mambo ya kutafuta haki za wanawake, wala akili ya mwanamke ijipange kukupambana na mwanaume.
Haya yote yametokea kwa sababu wanaume wamekuwa wakatili kwa wanawake, wanatumia nguvu na uwezo walionao kumuumiza na kumkandamiza mwanamke. Kwa sababu hiyo sasa kila mwanamke anayejua kufikiria amekaa mkao wa kukabidhiana na mwanaume mwonevu, na mwanaume hawezi kukubali kushindwa hata siku moja. Kwa gharama yoyote lazima awe juu. Ndio maana tunaona matatizo ya mahusiano na ndoa yanazidi kila siku.
Kwa hiyo sasa Wanaume wapendeni wake zenu, treat them gud, acheni tamaa mbaya, na uonevu, acheni mfumo dume wa kumkandamiza mwanamke.