MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
Ili uwe au u-qualify kuwa tajiri unatakiwa uwe na nini? Pisi kali nyingi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi siyo tajiri ila mwaka huu mwanzoni nilipata bahati ya kukutana na wafanyabiashara wachache wa Tanzania wenye mafanikio ambao tunaweza kuwaita matajiri. Nilishiriki kufanya survey ya benki ya dunia kuhusu viwanda vidogo na vya kati vinavyojishughulisha na utengenezaji na uchakataji wa mazao ya chakula.
Kitu ambacho nilijifunza kipindi chote nilipokuwa karibu na matajiri hao wote, wengi ni waoga wa kutoa taarifa sahihi walifanikiwa vipi, sababu kuu ni aidha wanaigopa serikali especially TRA pia wanahisi taarifa yeyote itakayotoka kwao ni siri ya biashara (trade secret) kitu ambacho si sahihi. Majority ya hawa watu ni over 35 years old. Dah! vijana tupo nyuma sana aisee. Mwisho kabisa hawa ni watu ambao wako busy sana katika ratiba zao za kila siku, unaweza kumtafuta wiki au mwezi usipate nafasi ya kuonana nae. Naomba niandike kwa kifupi stori kama tatu za baadhi ya wafanyabiashara hawa naamini kuna kitu tunaweza tukajifunza sote kwa pamoja.
1. Stori ya kwanza ni ya mama mmoja ambae yeye ni mmiliki wa kiwanda cha kuoka mikate na vitafunwa(Bakery). Mama huyu ana umri wa miaka zaidi ya 50 kwa kukadiria, yeye alikuwa mama wa nyumbani lakini baadae alijifunza ufundi cherehani na kuanza kushona. Anasema alikuwa akishona nguo kwa muda mrefu kabla kuja kuanzisha biashara ya bakery. Anasema katika eneo lake la kazi alipokuwa anaendelea na shughuli zake za ufundi kushona kulikuwa na bakery. Anasema fremu yake ilikuwa imepakana na hiyo bakery hivyo ikawa rahisi kwake kuzoeana na baadhi ya wafanyakazi wa hiyo bakery.
Basi kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele, akajikuta anatamani na yeye kuifanya ile bishara ya bakery. Tatizo likawa hajui aanzie wapi, basi ndipo alipomuuliza mmoja ya wafanyakazi wa ile bakery. Mfanyakazi yule akamwambia biashara ile ni rahisi unaweza kuanza hata ukiwa na mtaji mdogo, basi yule mama akaanza kukununua vifaa vyake vya bakery taratibu ambavyo alitumia kama miaka miwili kukamilisha set nzima ya kuanzia na vilikuwa na thamani ya almost Tsh 300,000. Basi anasema siku ya kwanza alifungua bakery yake nyumbani na alianza na mfuko mmoja tu wa Unga wa ngano akiwa na mfanyakazi mmoja tu. Then akiwa amekwisha anza ndo akaendelea na utaratibu wa kurasimisha biashara yake kwa maana ya kusajili leseni ya biashara, TFDA na BRELA.
Baada ya kuona demand ya bidhaa zake ni kubwa sana akaamua kuingia benki na kuomba mkopo wa vifaa na kuongeza uzalishaji katika kiwanda chake. Ndani ya miaka mitatu basi akawa amefanikiwa kupewa mkopo wa zaidi ya Tsh 100 milioni ambazo alipewa kama vifaa vya kutendea kazi. Kiwanda chake kilianza mwaka 2012 mwishoni akiwa na mfanyakazi mmoja lakini sasa hivi ameajiri vijana kama 20 hivi wengi wao ni kutoka VETA. Pia ameajiri mfanyakazi wa muda(part time) mkaguzi wa mahesabu ambaye anakagua pamoja na kumpa ushauri wa mambo ya kifedha katika biashara yake.
Itaendelea.....
To be honestly kwa mganga ,ila si kwamba alinipatia mamilioni no alinipanga sawa na nikaanza na biashara ya kawaida ila baadae daaah AHSANTE MUNGU ,AHSANTE MGANGA wa kweli. Dunia ina mambo kufanikiwa kuna njia nyingi sana
Hapa litakufa JITU!To be honestly kwa mganga ,ila si kwamba alinipatia mamilioni no alinipanga sawa na nikaanza na biashara ya kawaida ila baadae daaah AHSANTE MUNGU ,AHSANTE MGANGA wa kweli. Dunia ina mambo kufanikiwa kuna njia nyingi sana