kituli one
JF-Expert Member
- Feb 25, 2014
- 409
- 307
Ni aina gani ya Pikipiki ni nzuri kwa kufanyia biashara ya Bodaboda? Na vipi kuhusu bei zake?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
t-better mkuu
Nawezaje kujua boxer bm 150 kama ni orijino?Unapotafuta Pikipiki kwa ajili ya kufanyia biashara unapaswa kuzingatia kwanza mambo yafuatayo.
1/MAZINGIRA(Aina ya barabara, Je ni Lami au Changarawe, Tambarare au milima/mitelemko, mjini au kijijini nk.)
2/UTAMADUNI(Kila mahali kuna aina ya pikipiki inayofahamika na kupendwa na madereva na wateja)
3/VIPURI(Pikipiki ina matengenezo mengi madogo madogo kila mara, hivyo hakikisha vipuri vyake ni vinapatikana kwa urahisi, nafuu na Imara).
4/NGUVU(Kuna za 125cc(Nguvu ya kawaida, mafuta kawaida) na 150cc(ina nguvu zaidi, mafuta zaidi kidogo na bei juu kidogo). Kwa biashara ya boda boda 150cc inafaa zaidi kwa kuwa inahimili mzigo mzito kidogo)
BAADHI YA PIKIPIKI ZINAZOTUMIKA KWA BODA BODA.
(a)KINGLION(Inafaa popote, Ni nzito, ngumu na Imara. Bei 1.7milion)
(b)FEKON(Inafaa popote, ni nzito, ngumu na Imara.Bei 1.7milion)
(c)TOYO(Inafaa popote, ni nzito, ngumu, imara. Bei 1.7milion)
(d)SKYGO (Inafaa barabara zote lakini haifai milimani, ni imara lakini sio ngumu sana. Bei 1.6milion)
(e)BOXER (Inafaa mjini tena kwenye barabara nzuri, ni Lexury. Bei 2.2milion. Ndio pikipiki yenye kupendwa zaidi na wateja wa mjini, nyepesi, haina kelele wala moshi. Vipuri vyake ni ghali zaidi. Haifai vijijini au kubeba mizigo)
*Makampuni mengi siku hizi(Kinglion, Fekon, Skygo, Toyo) yametoa pia matoleo ya pikipiki zenye muundo na mwonekano wa boxer(Luxury) bei 2milion hivyo usishangae.
Zipo kampuni nyingi sana zenye majina tofautitofauti ambazo zijazitaja hapo kama Honda, Shineray, Huawang nk.
Binafsi sina uzoefu wowote wa kuweza kutofaitisha pikipiki origino na Fake, kifupi sijui kama pikipiki Fake za boxer kama zipo au la. ila kwa kukusaidia tu, zingatia haya unapotaka kununua pikipiki.Nawezaje kujua boxer bm 150 kama ni orijino?
Yapo maduka mengi sana kwa Dar yanayouza hizo pikipiki, kwa kukusaidia tu, mitaa ya Kariakoo karibu yote imejaa hayo maduka, pia kinondoni, temeke, Magomeni, Tabata nkHyo king lion napataje kwa hapa dar ninapesa cash?
Baada ya maelezo haya,Unapotafuta Pikipiki kwa ajili ya kufanyia biashara unapaswa kuzingatia kwanza mambo yafuatayo.
1/MAZINGIRA(Aina ya barabara, Je ni Lami au Changarawe, Tambarare au milima/mitelemko, mjini au kijijini nk.)
2/UTAMADUNI(Kila mahali kuna aina ya pikipiki inayofahamika na kupendwa na madereva na wateja)
3/VIPURI(Pikipiki ina matengenezo mengi madogo madogo kila mara, hivyo hakikisha vipuri vyake ni vinapatikana kwa urahisi, nafuu na Imara).
4/NGUVU(Kuna za 125cc(Nguvu ya kawaida, mafuta kawaida) na 150cc(ina nguvu zaidi, mafuta zaidi kidogo na bei juu kidogo). Kwa biashara ya boda boda 150cc inafaa zaidi kwa kuwa inahimili mzigo mzito kidogo)
BAADHI YA PIKIPIKI ZINAZOTUMIKA KWA BODA BODA.
(a)KINGLION(Inafaa popote, Ni nzito, ngumu na Imara. Bei 1.7milion)
(b)FEKON(Inafaa popote, ni nzito, ngumu na Imara.Bei 1.7milion)
(c)TOYO(Inafaa popote, ni nzito, ngumu, imara. Bei 1.7milion)
(d)SKYGO (Inafaa barabara zote lakini haifai milimani, ni imara lakini sio ngumu sana. Bei 1.6milion)
(e)BOXER (Inafaa mjini tena kwenye barabara nzuri, ni Lexury. Bei 2.2milion. Ndio pikipiki yenye kupendwa zaidi na wateja wa mjini, nyepesi, haina kelele wala moshi. Vipuri vyake ni ghali zaidi. Haifai vijijini au kubeba mizigo)
*Makampuni mengi siku hizi(Kinglion, Fekon, Skygo, Toyo) yametoa pia matoleo ya pikipiki zenye muundo na mwonekano wa boxer(Luxury) bei 2milion hivyo usishangae.
Zipo kampuni nyingi sana zenye majina tofautitofauti ambazo zijazitaja hapo kama Honda, Shineray, Huawang nk.
FEKONNi aina gani ya Pikipiki ni nzuri kwa kufanyia biashara ya Bodaboda? Na vipi kuhusu bei zake?
KARIBU MKUU ILA UTUPE HATA LIFT BASIIAsanteni wachangiaji wote kwa elimu iliyotukuka
Chukua t-better...mi nnayo miaka miwili saiv sijagusa engine wala chasis haijapinda inapiga mzigo naiita climberHyo king lion napataje kwa hapa dar ninapesa cash?
Kampuni gani inakopesha bajajiKama unataka ununue pikipiki uendeshe mwenyewe nakushauri ununue boxer(2,000,000) bshaka utakua makini kwenye uendeshaji,usafi,matunzo na service. Lakini kama mpango wako ni kununua na kumpa mtu akuendeshee nakushauri ununue SUNLG(1,800,000) au FEKON(1,650,000).
Kununua Boxer alafu ukampa mtu akuendeshee naomba nikwambie kuwa hiyo pesa yako kamwe haitorudi kwan itawahi kuharibika kabla ya kurejesha mtaji na faida. BOXER ya miezi 6 ukiiona haitamaniki na hasa hawa madreva dizaini ya akina mcharo ndo kabisaa mwaka haimalizi ushapeleka dampo. Otherwise hii biashara ya bodaboda utapata pesa kama unaendesha mwenyewe ila kumpa mtu aendeshe inakula kwako.
Kama una 2.5mln unaweza kupata Bajaj ya mkopo... ukawa unarejesha taratibu ndani ya miezi 6 umemaliza unaanza kula pesa tu. Jiulize misimu ya mvua kama hii nani anapanda bodaboda? Wengi wameenda likizo. Ni hayo tu.