Ni pikipiki gani nzuri kwa biashara ya Bodaboda?

Ni pikipiki gani nzuri kwa biashara ya Bodaboda?

Kama unataka ununue pikipiki uendeshe mwenyewe nakushauri ununue boxer(2,000,000) bshaka utakua makini kwenye uendeshaji,usafi,matunzo na service. Lakini kama mpango wako ni kununua na kumpa mtu akuendeshee nakushauri ununue SUNLG(1,800,000) au FEKON(1,650,000).

Kununua Boxer alafu ukampa mtu akuendeshee naomba nikwambie kuwa hiyo pesa yako kamwe haitorudi kwan itawahi kuharibika kabla ya kurejesha mtaji na faida. BOXER ya miezi 6 ukiiona haitamaniki na hasa hawa madreva dizaini ya akina mcharo ndo kabisaa mwaka haimalizi ushapeleka dampo. Otherwise hii biashara ya bodaboda utapata pesa kama unaendesha mwenyewe ila kumpa mtu aendeshe inakula kwako.

Kama una 2.5mln unaweza kupata Bajaj ya mkopo... ukawa unarejesha taratibu ndani ya miezi 6 umemaliza unaanza kula pesa tu. Jiulize misimu ya mvua kama hii nani anapanda bodaboda? Wengi wameenda likizo. Ni hayo tu.
Kwa hoja hizi naweka vema. Na mjadala ufungwe. Nina uzoefu wa pikipiki tangu 2003
 
Back
Top Bottom