Ni Rahisi Kupoteza Biashara Yako Kama Hautailinda Kisheria

Ni Rahisi Kupoteza Biashara Yako Kama Hautailinda Kisheria

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,811
Reaction score
3,888

Jinsi Nilivyomsaidia Mteja Wangu Kumsajilia Jina la Biashara​


Nilipokutana na mteja wangu kwa mara ya kwanza, alikuwa amechoka na mawazo akijaribu kuanzisha biashara yake. Alikuwa na ndoto, wazo, na hata jina la biashara alilopenda lakini hakuwa na ufahamu kamili wa taratibu rasmi za kulisajili kupitia BRELA.

Ndipo nilipochukua jukumu hilo kwa mikono miwili kumsaidia katika kuanzisha biashara yake.

Tulianza kwa hatua ya kwanza muhimu​

kufanya utafiti wa jina.​

Nilihakikisha jina alilochagua bado halijatumika. Nilimwonyesha jinsi ya kuangalia kupitia tovuti ya BRELA, lakini nikaenda mbele zaidi: nilitumia uzoefu wangu kufanya ulinganifu wa majina yanayofanana sokoni ili kuhakikisha tunamtengenezea personal brand.

Huu ndio msingi wa biashara kujitofautisha mapema.

Baada ya hapo, nilimfungulia akaunti katika mfumo wa BRELA Online Registration System (ORS).​

Hii si hatua ya moja kwa moja kwa watu wengi, hasa wale wasiozoea mifumo ya kidijitali. Nilimsaidia kujaza taarifa muhimu kuanzia shughuli halisi za biashara yake, hadi maelezo ya anwani na mawasiliano.

Tulihakikisha kila kitu kimejazwa kwa usahihi, tukiepuka makosa ambayo yangeweza kuchelewesha mchakato.

Kisha tuliendelea na kulipa ada ya usajili.​

Nilimshauri juu ya njia salama na halali za malipo mtandaoni, nikahakikisha kila hatua inathibitishwa kwa risiti na rekodi kamili. Kwa kuwa biashara ilikuwa bado changa, nilimsaidia pia kuandaa baadhi ya nyaraka za awali alizohitaji kuweka kwenye mfumo.

Hatimaye​

Baada ya kusubiri kwa siku chache, nilimpigia simu kumweleza kuwa cheti chake cha usajili kimetoka.

Kwa mara ya kwanza, biashara yake ilikuwa imetambulika rasmi kisheria na jina lake sasa lilikuwa limelindwa dhidi ya mtu mwingine kulitumia kiholela.

Lakini msaada wangu haukuishia hapo.​

Nilimweleza kwa kina faida za hatua aliyochukua:

  1. Biashara yake sasa inaweza kufungua akaunti ya benki na njia za malipo kwa jina la kampuni.
2. Anaweza kuomba leseni, mikopo, na kushirikiana na taasisi kubwa bila kubaguliwa.

3. Wateja wake wataanza kumuona kama mtoa huduma halali, si tu muuzaji wa mitaani.

4. Na muhimu zaidi, biashara yake ilikuwa imepata utambulisho rasmi na ulinzi wa kisheria.

Siku hiyo tulimaliza kwa kinywaji pale wag hills, lakini kwangu, ushindi mkubwa ulikuwa si tu usajili wa jina bali kuiona ndoto ya mtu ikianza kupata na kufanya biashara halisi.

Ikiwa na wewe unahitaji msaada kama huu, usisite kunitafuta kupitia WhatsApp: wa.me/+255693880325

1*H8FuxzXUTcr4ovKUNqW38A.jpeg


Nipo hapa kuhakikisha jina la biashara yako si ndoto tu, bali hatua ya kwanza ya mafanikio yako ya kibiashara.
 
Hongera mkuu, ila hili ni tangazo lako la kwamba "Unatoa Msaada wa Kusajili Kampuni za Kibiashara"
 
Back
Top Bottom