Ni Rasmi sasa kiwanda cha magari ya Volkswagen chafunguliwa Kenya

Hongera majirani... Sisi tuna kazania hivi vya kufyatua watoto na matofali kwanza.
 
Kwanini hawakukijenga Tz badi kama ndio soko walilolilenga?
Walikuja kutaka kuwekeza hapa kwanza kabla ya Kenya kupitia mwamvuli wa SADC, hatukuelewana nao maswala mbalimbali ndio wakachomokea huko.
 
Walikuja kutaka kuwekeza hapa kwanza kabla ya Kenya kupitia mwamvuli wa SADC, hatukuelewana nao maswala mbalimbali ndio wakachomokea huko.
Kwahiyo tunakubaliana kwamba inchi hii haina sera rafiki kwa uwekezaji?
 
Kwahiyo tunakubaliana kwamba inchi hii haina sera rafiki kwa uwekezaji?
Kwa upande wangu mimi sikubaliani na kwamba hatuna sera nzuri ya uwekezaji. Sera ya zamani ya tax holiday imetufikisha tulipo hapa, haifai gia lazima zibadilishwe angani. Mtu aliye kuja kukusaidia kujenga nyumba mwisho wa siku anakuambia nipe watoto wako wote na nguo zako, huyo sio mtu wa kukusaidia amekuja kujitajirisha tuu.
 
Sis tupo bize kufufua viwanda vilivyokufa
 
Lile track la kichina tulisema tutalizundua kibaha December hivi inatakiwa kuwa tarehe ngapi vile?
 
Binafsi sitaki kuamini kwamba swala la tax holiday kama ndio kigezo kikuu kilichopelekea kushindikana kwa maelewano baina ya serikali ya Tanzania na kampuni ya VW.Kiufupi watu tuliowapatia dhamana licha ya kujinasibu na dira ya kutupeleka katika uchumi wa viwanda, wameshindwa kutuonyesha kwa uhalisia ni jinsi gani tutafika huko pasipo kuwa na sera na mbinu stahiki zitakazoweza kuchochea ujio wa wawekezaji kutoka nje kuleta mitaji yao hapa kwetu na sio kwa inchi jirani tunazo shindana nazo kiuchumi na kimaendeleo.Baada ya sisi kushindwa ilikuwa obvious wakenya wasingemuachia muwekezaji huyu.Pia tusisahau mahusiano ya kibiashara kati ya serikali ya Kenya na VW.Kama rekodi zangu zipo sahihi, Rais Kenyata wakati akiwa waziri wa Fedha chini ya utawala wa Rais Mwai Kibaki, aliwahi kufanya manunuzi ya VW Passat kwa Viongozi wa umma lengo likiwa ni kubana matumizi kwa kuondokana na matumizi ya "mashangingi".Inchi hii tunahitaji viongozi sio tu wenye taaluma, bali wawe pia na weledi na mbinu za kushawishi wawekezaji.Lengo haliwezi kutimia pasipo kuwa na lobbying!
 
Kwanza kabisa labda niweke bayana kuwa nilipo zungumzia kuhusu tax holiday sikuwa nazungumzia jinsi VW walivyo geuza njia na kugonga mlango wa jirani. Nilikuwa nazungumza jinsi tunakuwa tunajitolea mpaka nafsi zetu kuwapendezesha wawekezaji mwisho wa siku ndio sisi tunabaki masikini na omba omba. Sasa tukija kwenye sera, sera Tanzania zipo, labda sio kali kama wengi tutakavyo penda ziwe, lakini zipo. Ila, hapa kwetu hatunaga utamaduni wa kuzitangaza, utazikuta zipo huko wizarani au kweye idara fulani zinakanata vumbi. Nakumbuka Rais wa China alipokuja Tanzania akasaini mikataba 19, mmoja kati ya mkataba hiyo ilikuwa ni wa kufunguliwa soko huru la kupeleka tumbaku China. Ktk Africa ni Tanzania na Zimbabwe tuu ndio wanamkataba kama huo. Na hakuna nchi duniani inaongoza kuvuta sigara kama China. Lakini huo mkataba uko wapi, upo maofisi unakamata vumpi. Udhahifu unaanza na viongozi tuliowapa dhamana ya kuhoji (wabunge), wao ndio wange weza kuchokonoa yote haya na kutuchambulia sisi makabwela tujuwe kinacho endelea. Ukitegemea serikalini kuja kutuwekea chakuka midomoni na kututafunia, tuta lala na njaa.
Dira ya uwekezaji duniani imebadilika sana, zamani wawekezaji walikuwa wanaringa, lazima uwape lundo la zawadi kama tax holiday ndio waje kuwekeza kwako. Lakini siku hizi wawekezaji wana hela nyingi na maoneo ya uwekezaji yamepungua, kwasababu nchi zinazoonyesha dalili ya uchumi unaokaribia au kuzidi asilimia 6-7 ni chache duniani. Miaka kumi iliyopita usinge muona VW anakimbilia kufungua kiwanda kwenye nchi kama zatu, kwasababu huko huko wanapokuwa wanazalisha zamani kulikuwa kunatosha. Sasa hivi inabidi washindane na nchi kama Korea, Indian, Poland au hata China. Kwa hiyo tusijilaumu sana kwa kukosa kampuni kama hii VW, bado zipo kampuni nyingi tuu na zinakuja. Na sio lazima ziwe za magari, vipo vitu vingi vya kutengeneza msjiko, vifaa vya hospitali, viyoyozi nk. Uchumi wa gesi asilia hauwezi kulinganishwa na uchumi mwingine duniani. Wewe Google bidhaa zinazotokana na natural gas uone ni nini tunaweza kuzalisha.
 

Very good points mkuu. Yaani wachangiaji wengi wangekuwa kama wewe, tungekuwa mbali sana.
 
Kuanzisha kiwanda sio issue kubwa,issue hapo ni je Africa mashariki how many people can buy brand new car? Watauza ulaya yaliko mengi? au america? Au japani?Vitz yenyewe mpya m 30,je hizo voks? Ngoja tusubiri tuone,mwanzoni si walisitisha?
 
Tatizo Tanzania yetu wapiga deal wengi mfano kwa dangote anatakiwa anunue makaa ya mawe ya hapa lkn wakawa wanamnunulisha ya kutoka south afrika
 
Acha kutisha watu hapa hata kama ni mvaa suti nyeusi.. Rubbish.
Hao wanaotishia watu wasitoe mawazo yao ndo mijitu ambayo ina roho za kwa nini na isiyopenda kusikia ukweli sasa hapo rais kasemwa wapi uwe unajiheshimu bhn kubwa zima busara huna
 
Kuanzisha kiwanda sio issue kubwa,issue hapo ni je Africa mashariki how many people can buy brand new car? Watauza ulaya yaliko mengi? au america? Au japani?Vitz yenyewe mpya m 30,je hizo voks? Ngoja tusubiri tuone,mwanzoni si walisitisha?
point hyo mkuu[emoji122] [emoji122]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…