Binafsi sitaki kuamini kwamba swala la tax holiday kama ndio kigezo kikuu kilichopelekea kushindikana kwa maelewano baina ya serikali ya Tanzania na kampuni ya VW.Kiufupi watu tuliowapatia dhamana licha ya kujinasibu na dira ya kutupeleka katika uchumi wa viwanda, wameshindwa kutuonyesha kwa uhalisia ni jinsi gani tutafika huko pasipo kuwa na sera na mbinu stahiki zitakazoweza kuchochea ujio wa wawekezaji kutoka nje kuleta mitaji yao hapa kwetu na sio kwa inchi jirani tunazo shindana nazo kiuchumi na kimaendeleo.Baada ya sisi kushindwa ilikuwa obvious wakenya wasingemuachia muwekezaji huyu.Pia tusisahau mahusiano ya kibiashara kati ya serikali ya Kenya na VW.Kama rekodi zangu zipo sahihi, Rais Kenyata wakati akiwa waziri wa Fedha chini ya utawala wa Rais Mwai Kibaki, aliwahi kufanya manunuzi ya VW Passat kwa Viongozi wa umma lengo likiwa ni kubana matumizi kwa kuondokana na matumizi ya "mashangingi".Inchi hii tunahitaji viongozi sio tu wenye taaluma, bali wawe pia na weledi na mbinu za kushawishi wawekezaji.Lengo haliwezi kutimia pasipo kuwa na lobbying!