Ni sababu gani zilipelekea chama cha TANU kubadili jina mwaka 1977?

Ni sababu gani zilipelekea chama cha TANU kubadili jina mwaka 1977?

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
kwa wanaoelewa sababu zilizopelekea chama cha TANU kugeuzwa kuwa Chama Cha Mapinduzi anijuze tafadhari maana mimi kama mimi sioni haja ya TANU kuwa chama cha mapinduzi.
 
kwa wanaoelewa sababu zilizopelekea chama cha TANU kugeuzwa kuwa Chama Cha Mapinduzi anijuze tafadhari maana mimi kama mimi sioni haja ya TANU kuwa chama cha mapinduzi
Kwani vipi Kaka, una wasiwasi na Chama kubwa sana TZ kuliko vyote "CCM" kuwa Wanyonge tulipigwa na bado tunaendelea kupigwa na kitu kizito tangu tupate uhuru 1964 [emoji848][emoji16]
 
kwa wanaoelewa sababu zilizopelekea chama cha TANU kugeuzwa kuwa Chama Cha Mapinduzi anijuze tafadhari maana mimi kama mimi sioni haja ya TANU kuwa chama cha mapinduzi
Ni kwamba kabla ya mwaka 1977 Tanzania ilikuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Lengo la Vyama vingi vya siasa ni kuchochea maendeleo ya wananchi kwa vyama hivi kuibua mawazo tofauti tofauti ya jinsi ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Lakini enzi hizo vyama vya siasa vilijikita katika kugombania madaraka kwa kutumia mbinu "chafu". Wapo walioshawishi wananchi wasishiriki katika shughuli za maendeleo, wapo waliotengeneza fitina, wapo walioshawishi wananchi kulaani maendeleo, wapo waliokuwa tayari kuungana tena na wakoloni ilimradi wao wapate madaraka.

Kwa wanasiasa walioshindania madaraka hii waliita demokrasia kuwa inawaruhusu kufanya chochote kutafuta madaraka.

Kwa watala wa enzi hizo, huu ulionekana ujinga uliopitiliza kuwa upumbavu na waliona busara ni kufuta mfumo wa vyama vingi vya siasa. Kabla ya hapo TANU walikuwa wametengeneza ahadi zilizolenga kuwadhibiti watu wao kutojiingiza katika siasa chafu.

Ili kuonekana chama kimoja hakikufuta vyama vingine na kubaki chenyewe nadhani ilikuwa ni njia moja wapo ni kubadili jina na hivyo tunaweza kusema TANU siyo CCM.

Kigezo kilichotumika kuchagua jina CCM nadhani historia niliyojifunza haikuweka bayana.

Na changamoto kubwa tuliyokumbana nayo baada ya kurejea kwenye mfumo wa vyama vingi ni kutokuweka misingi imara imayotuelekeza katika kutorudia makosa yaliyokuwa yakifanyika miaka hiyo kupitia mwavuli wa vyama vingi.

Tunaanza kushuhudia mambo yaleyale ya siasa za vyama vingi kugeuka fitna na mambo mengine na hapa ni kuweka wazi kuwa sheria ya siasa za vyama vingi ni muhimu sana cha msingi isitumike yenyewe kutengeneza siasa chafu bali kuleta siasa safi
 
Mkuu
Siyo RASMI
Mwl NYERERE ni zao la seminary
Lazima atumikie kanisa KWA nembo ya kanisa

Catholic church movement:-ccm

TANU hakikuwa chombo cha kanisa

CCM ni Dini siyo CHAMA cha SIASA

Inalindwa na TISS ambayo ofisi zao baadhi zipo st peters!!!

Hayo ni maneno ya wazee wa zamani vijiweni

Siyo RASMI

Kuna siri kubwa za WAZEE
Ndio Hivyo!!
 
kwa wanaoelewa sababu zilizopelekea chama cha TANU kugeuzwa kuwa Chama Cha Mapinduzi anijuze tafadhari maana mimi kama mimi sioni haja ya TANU kuwa chama cha mapinduzi
Ukisoma sheria ya vyama vya siasa Tanzania hairuhusu chama kuwa cha upande mmoja tu wa Muungano.

South Africa wana mpaka vyama vya kikabila cha Inkhata Freedom party kipo Kwazulu Natal cha Chief Mangosuthu Buthelezi, hiki ni chama cha Wazulu pasee.
 
Huyu Mangesuthu Bhuthelezi si ndiye alikuwa puppet wa Makaburu na alichangia sana kupatikana kwa uchaguzi wa wote Afrika ya Kusini
 
Kwa nini jina libadilishwe kuwa chama cha mapinduzi

..niliwahi kusikia kwamba wakati wanatafuta jina la chama kipya Waznz walisisitiza kwamba mapinduzi ya Znz lazima yaenziwe hivyo likapatikana jina la " chama cha mapinduzi. "

..sina uhakika kama taarifa hizo ni za kweli, hivyo nakushauri uzifanyie uhakiki.
 
Kwa mujibu wa mzee mihangwa ndivyo ilivyokua,mzee mihangwa ni 'mbeba makabrasha kipindi hicho'....nadhani umenielewa
 
Back
Top Bottom