kwa wanaoelewa sababu zilizopelekea chama cha TANU kugeuzwa kuwa Chama Cha Mapinduzi anijuze tafadhari maana mimi kama mimi sioni haja ya TANU kuwa chama cha mapinduzi
Ni kwamba kabla ya mwaka 1977 Tanzania ilikuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Lengo la Vyama vingi vya siasa ni kuchochea maendeleo ya wananchi kwa vyama hivi kuibua mawazo tofauti tofauti ya jinsi ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Lakini enzi hizo vyama vya siasa vilijikita katika kugombania madaraka kwa kutumia mbinu "chafu". Wapo walioshawishi wananchi wasishiriki katika shughuli za maendeleo, wapo waliotengeneza fitina, wapo walioshawishi wananchi kulaani maendeleo, wapo waliokuwa tayari kuungana tena na wakoloni ilimradi wao wapate madaraka.
Kwa wanasiasa walioshindania madaraka hii waliita demokrasia kuwa inawaruhusu kufanya chochote kutafuta madaraka.
Kwa watala wa enzi hizo, huu ulionekana ujinga uliopitiliza kuwa upumbavu na waliona busara ni kufuta mfumo wa vyama vingi vya siasa. Kabla ya hapo TANU walikuwa wametengeneza ahadi zilizolenga kuwadhibiti watu wao kutojiingiza katika siasa chafu.
Ili kuonekana chama kimoja hakikufuta vyama vingine na kubaki chenyewe nadhani ilikuwa ni njia moja wapo ni kubadili jina na hivyo tunaweza kusema TANU siyo CCM.
Kigezo kilichotumika kuchagua jina CCM nadhani historia niliyojifunza haikuweka bayana.
Na changamoto kubwa tuliyokumbana nayo baada ya kurejea kwenye mfumo wa vyama vingi ni kutokuweka misingi imara imayotuelekeza katika kutorudia makosa yaliyokuwa yakifanyika miaka hiyo kupitia mwavuli wa vyama vingi.
Tunaanza kushuhudia mambo yaleyale ya siasa za vyama vingi kugeuka fitna na mambo mengine na hapa ni kuweka wazi kuwa sheria ya siasa za vyama vingi ni muhimu sana cha msingi isitumike yenyewe kutengeneza siasa chafu bali kuleta siasa safi