GIPAMA
JF-Expert Member
- May 21, 2016
- 1,103
- 541
Madaktari mlioko humu naomba kuuliza, ni sababu zipi za kisayansi ambazo humfanya mwanamke mjamzito atapike!?
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Front seat: tayari imeshanyunyiziwa maziwa mepesi yakaleta virutubisho ndani ya Fallopian tubes hongeraMadaktari mlioko humu naomba kuuliza, ni sababu zipi za kisayansi ambazo humfanya mwanamke mjamzito atapike!?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mchango wako plz kapalamsenga.Front seat: tayari imeshanyunyiziwa maziwa mepesi yakaleta virutubisho ndani ya Fallopian tubes hongera
Sent using Jamii Forums mobile app
Mwanamke akipata Mimba hafu anatapika, au kuacha kula vyakula Fulani hapo huwa naita Mimba jiwe, maana ile sperm iliyoingia katika yai ilikuwa na nguvu na afya ya kutosha na maranyingi mtoto wa kiume huzaliwaKimsingi hii hali ni ya kawaida kwa wanawake wanaokuwa katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito though hutofautina kati ya mwanamke mmoja na mwingine. Wengine hutapika sana kiasi cha kuhitaji kupaatiwa msaada wa kitabibu au hata kulazwa kabisa (hali hii huitwa Hyperemesis gravidarum) hii ni mbaya sana kwa afya ya mama na mtoto wake, kwa wengine ni kwa kiasi tu hivyo kutokua na madhara kwao na hupotea baada ya miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito. Hali hii huitwa Morning sickness kama ni kwa kiasi !
Sababu kamili hazijulikani ila kuna nadharia hizi nadhani zinajaribu kufafanua vizuri:
1. Mabadiliko ya vichocheo vya mwili (homoni): Hasa hasa hii human chorionic gonadotropin (hCG) hii huwa inaongeza athari katika sehemu ya maalumu inayocontrol kutapika (emetic center)kwenye ubongo pia hCG inaifanya tezi ya thyroid iliyopo shingoni kuzalisha vichocheo vyake ambazo huwa na athari kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kwa kuongeza kasi ya utumbo kuwa motile au kusukuma chakula. Nyingine huitwa serotonin nayo ina madhara kama yalivyotajwa hapo juu
2. Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula: Helicobacter pylori bacteria anayeishi kwenue utumbo husababisha madonda ya tumbo(peptic ulcer disease). Bacteria hawa hukutwa kwa kiasi kikubwa kwa wakina mama wajawazito wenye kutapika sana wakati wa ujauzito.
3. AKILI: Ingawa hii nadharia huchanganya sana, watafiti wengine huona ni kama swala la kijamii zaidi pale mwanamke anapokua mjamzito hujitahidi kupambana na hali ile ya ujauzito, so wao wanaprefer counselling tu kama tiba ya kuzuia kutapika.
Sent using Jamii Forums mobile app
Doh haya nasubiria dume sio kwa kutapika huku na kubagua vyakulaMwanamke akipata Mimba hafu anatapika, au kuacha kula vyakula Fulani hapo huwa naita Mimba jiwe, maana ile sperm iliyoingia katika yai ilikuwa na nguvu na afya ya kutosha na maranyingi mtoto wa kiume huzaliwa
Sent using Jamii Forums mobile app
Naona wanaJF wengi tumeuamulia mwaka huu.Doh haya nasubiria dume sio kwa kutapika huku na kubagua vyakula
Hatutaki mchezo mchezoNaona wanaJF wengi tumeuamulia mwaka huu.
Hongera.
Sasa HV naenda mwezi wa tano, nimepunguza kutapika kidogo. Sio kama mwanzoniUnapata/anapata dalili gan kwa miez ip